• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri mkuu wa China barani Latin Amerika yafungua njia mpya ya ushirikiano kati ya China na bara hilo

    (GMT+08:00) 2015-05-29 17:48:19

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo asubuhi amerudi Beijing baada ya kumaliza ziara yake katika nchi za Brazil, Colombia, Peru na Chile.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipozungumzia ziara hiyo ya Bw. Li Keqiang amesema imefungua njia mpya ya ushirikiano kati ya China na Latin Amerika, kupanua mustakabali mpya wa ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kutafuta njia mpya ya ushirikiano kati ya Kusini na Kaskazini.

    Bw. Wang Yi amesema wakati wa ziara ya rais Xi Jinping wa China katika nchi za Latin Amerika mwaka jana, pande hizo mbili zimethibitisha kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wenye kunufaishana na kuendelea kwa pamoja, na ziara ya Bw. Li Keqiang imesukuma mbele uhusiano huo, na kupata mafanikio mengi halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako