• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliofariki kutokana na joto kali nchini India yafikia 1,700

    (GMT+08:00) 2015-05-29 19:00:21

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na joto kali nchini India katika wiki moja iliyopita imefikia 1,700.

    Vifo vingi vimetokea kwenye mikoa ya kusini ya Andhra Pradesh na Telangana, ambapo katika mkoa wa Telangana pekee, watu 100 wamefariki kutokana na joto kali katika saa 24 zilizopita. Kiwango cha joto katika mikoa hiyo miwili kimefikia nyuzi 47, huku halijoto kwenye mji mkuu wa Infia ikifikia nyuzi 45.

    Vifo pia vimeripotiwa katika mkoa wa magharibi wa Gujarat, ambapo inasemekana kuwa watu wengi waliofariki ni wale wasio na makazi na vibarua. Mamlaka ya hali ya hewa nchini India imetabiri kuwa, joto kali litaendelea nchini India kwa siku mbili zaidi.

    Serikali katika mikoa ya kusini imewataka watu wasitoke nje wakati wa jua kali, na maofisa wa afya wamependekeza watu wanywe maji kwa wingi kabla ya kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako