• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukamilisha sera kuhusu uagizaji bidhaa kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya wateja wa ndani

    (GMT+08:00) 2015-05-29 19:22:07

    China itapunguza kwa nusu kiwango cha ushuru kwa baadhi ya bidhaa za matumizi ya kila siku zinazoagizwa kutoka nje, zikiwemo nguo, viatu na vipodozi. Lengo la hatua hiyo ni kukidhi mahitaji ya wateja na kuhimiza matumizi ya ndani. Mbali na kupunguza ushuru, China pia itatoa sera mbalimbali za kurahisisha biashara na kuongeza idadi ya maduka yasiyotoza kodi.

    Hatua hii mpya inahusisha bidhaa nyingi amabazo wateja wa China wanapenda kununua wanapotembelea nchi za nje. Naibu waziri wa fedha wa China Bw. Shi Yaobin amesema, hatua hiyo hailengi nchi fulani maalumu, na wala hailengi kuvutia wachina wafanye manunuzi nchini baadala ya nchi za ng'ambo, bali inalenga kukidhi mahitaji ya wateja wa China kwa bidhaa za aina mbalimbali.

    "Sera za ushuru na sera nyingine za kurahisisha biashara zilizoamuliwa kwenye mkutano wa Baraza la serikali zinalenga kukidhi mahitaji ya wateja wa China kwa bidhaa za aina nyingi na kuongeza aina za bidhaa kwenye soko la ndani. Kwa kawaida kupunguza ushuru kwa baadhi ya bidhaa, kunaongeza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje, na kuongeza aina za bidhaa hizo sokoni, hivyo kurahisisha manunuzi ya wateja wa ndani. Kwa sababu baadhi ya watu wanatembelea nchi za nje, wengine hawajapata fursa ya kufanya hivyo, lakini pia wanaweza kupata bidhaa hizo zinazoagizwa kutoka nje moja kwa moja kwenye soko la China."

    Bw. Shi Yaobin amesema, hatua hiyo pia haihusishi malengo ya kifedha au kodi, na utekelezaji wa sera hizo utapunguza mapato ya ushuru wa forodha. Lakini amesema bado haijulikani ni kiasi gani kitakachopunguzwa kwa bidhaa zilizoagizwa kutoka nje.

    Mbali na ushuru, bei ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje pia inaathiriwa na mambo mengi, ikiwemo gharama za usafirishaji, mkakati wa bei tofauti kwenye kanda tofauti na gharama za usimamizi za kampuni zinazoingiza bidhaa hizo. Lakini ukweli ni kwamba, baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zinauzwa kwa bei ghali, sasa hatua gani zitahimiza kampuni zilizozalisha bidhaa hizo ziweke bei ya haki zaidi kwenye soko la China?

    Akizungumzia suala hilo, naibu waziri wa fedha wa China Bw. Wang Shouwen anaona, pengo hili litaendelea kupunguzwa, na sasa mwelekeo huo umeonekana sokoni.

    "Ushinda umekuwa mkali zaidi. Sasa kuna njia nyingi zaidi kwa chapa za kigeni kuingia China, zamani China haikuwa na majumba ya maduka ya Outlets, lakini sasa yako sehemu nyingi nchini. Ushindani ukiongezeka, bei ya chapa itashuka. Hayo ni matokeo ya China kufungua mlango kwa nje katika sekta ya biashara. Tumetekeleza sera mpya kwenye eneo la biashara huria mjini Shanghai, inayoruhusu kuagiza magari moja kwa moja kutoka nje, hatua ambayo pia imezidisha ushindani na kupunguza ukiritimba wa wakala wa chapa hizi za kigeni nchini China. Kutekelezwa kwa sera hizo pamoja na kujitokeza kwa chapa za kichina, na kupunguzwa kwa ushuru wa forodha, kumesaidia kupunguza tofauti za bei ya bidhaa sawa kwenye soko la China na soko la nje."

    Serikali ya China pia inapanga kuongeza idadi ya maduka yasiyotoza kodi kwenye bandari na forodha za kuingia China. Naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya forodha ya China Bw. Lu Peijun anasema,

    "Hakuna maduka mengi yasiyotoza kodi kwenye forodha za kuingia China, ila tu katika forodha kubwa katika miji ya Beijing, Shanghai, Shenzhen na Zhuhai. Kwa mujibu wa uamuzi wa Baraza la serikali ya China, safari hii tutaongeza maduka hayo, kwa hatua ijayo tutashirikiana na idara husika za wizara ya fedha kutekeleza kazi hiyo. Maduka yataongezwa kwenye forodha gani inatokana na nia ya makampuni na mahitaji ya forodha, na tutafanya tathmini zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako