• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji wamezea mate eneo la kericho kwa ajili ya ufunguzi wa kiwanda cha saruji

    (GMT+08:00) 2015-05-29 20:35:14

    Kiwanda cha saruji chenye uwezo wa kuzalisha tani 730,000 kwa mwaka kitafunguliwa eneo la kericho ili kuongeza ushindani katika sekta hiyo na kuleta utulivu wa bei.

    Kampuni ya Rai ya saruji ina mipango ya kujenga kiwanda cha mabilioni ya pesa katika ardhi ya ekari 50 ambayo iko katika kijiji cha Kaplelach ambayo ni kilomita 30 kutoka mjini Kericho.

    Itakuwa kiwanda cha kwanza cha saruji kufunguliwa katika mkoa wa magharibi mwa

    Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 2,000 ya saruji kwa siku kwa kutumia malighafi.

    Ongezeko la matumizi ya saruji nchini kenya na nchi jirani ambayo inaendeshwa na miradi mikubwa ya miundombinu imevutia wawekezaji wa kimataifa.

    Bw: Dangote,tajiri mkubwa barani Afrika, anasema anatarajia kuanzisha kiwanda cha zaidi ya sh bilioni 35 maeneo ya kitui na ambacho kina uwezo wakuzalisha tani milioni.

    Bw: Cemtech pia ana mipango ya kujenga kiwanda cha saruji chenye thamani ya Sh bilioni 10 maeneo ya Pokot na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka.

    Hivi sasa, Kenya ina wazalishaji wa saruji sita na Bamburi Cement ikifurahia soko kubwa.

    Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Kenya inaonyesha makampuni hayo sita yalizalisha tani milioni 5.8 za saruji mwaka jana kutoka tani milioni tano mwaka uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako