• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera ya gesi asilia kuwafaidi wote

    (GMT+08:00) 2015-05-29 20:35:49

    Sera ya kuhakikisha watu wa kawaida wanafaidika na utafutaji wa gesi asilia nchini imekuwa tayari na hivi karibuni itaanza kutumiwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw Godfrey Simbeye, imethibitisha.

    Serikali tayari imeweka na kupitisha sera na kuhakikisha Watanzania wanafaidika na maliasili.

    Kulingana na Bw Simbeye, sera ambayo itahakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika utafutaji wa rasilimali itaongozwa na bodi ya uongozi hadi utekelezaji wake.

    Akizungumzia baadhi ya walengwa, Bw Simbeye anasema kuwa Watanzania watakuwa na uwezo wa kupata mgao wa asilimia kutoka kwa makampuni ya kigeni ambayo yanawekeza katika gesi asilia.

    Sera hiyo pia itawawezesha wananchi wa kawaida kushirikiana na makampuni ya kigeni katika ngazi zote za mzunguko wa thamani.

    Hoja hii itawezesha wananchi kuwa na uwezo wa kupata ujuzi na maarifa, juu ya uvumbuzi kupitia wataalam wa kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako