• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ugatuzi kama hatua ya kuondoa urasimu

    (GMT+08:00) 2015-06-04 10:02:28

    Hivi sasa kuna mjadala unaoendelea hapa China kuhusu changamoto ndogo ndogo wanazokabiliana nazo watu wanapotafuta huduma kwenye idara za serikali. Kutokana na kufuata utaratibu kupita kiasi hata kwenye mambo madogo madogo, baadhi ya watu wanaona kuwa huu ni urasimu usiohitajika. Kwa Kiswahili neno urasimu lina maana mbili, kwanza maana yake ni utaratibu wa kufuata taratibu rasmi zilizoamuliwa na serikali, shirika, chama au idara yoyote. Na lengo ni kuhakikisha mambo hayafanyiki kiholela, hii ni maana nzuri. Lakini ya pili ni machungu yanayotokana na kufuata mlolongo wa mambo ambayo wakati mwingine yanachosha tu watu, na si ya muhimu sana, hata yakiachwa haina maana kuwa taratibu muhimu zimeharibiwa. Hii ni maana mbaya ya urasimu, na kwenye mjadala huu hayo ndiyo ambayo wenzetu hapa China wanaona kuwa yanatakiwa kuondolewa. Kwa undani zaidi hebu kusikiliza kipindi chetu.

     


    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako