• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kabila la mbilikimo barani Afrika liko hatarini kutoweka

    (GMT+08:00) 2015-06-11 14:02:15

    Kwenye sehemu za katikati ya Afrika, Kuna kabila moja maalumu la mbilikimo linaloaminiwa kuwa ni kabila la asili linaloishi kwenye kanda hiyo.

    Kabila la mbilikimo ni kabila la watu wafupi barani Afrika, pia kwa kiingereza wanaitwa kabila la Nigrillo, kwa wastani watu wazima wa kabila hilo wana urefu wa mita 1.3 hadi 1.4. Utafiti wa kianthropolojia umethibitisha kuwa watu wa kabila la mbilikimo ni warithi wa ustaarabu wa Sangha uliokuwepo kabla ya historia ya binadamu. Ingawa mbilikimo ni wafupi, lakini wana nguvu kubwa na wote ni wawindaji hodari na kujiita kuwa "watoto wa misitu".

    Watu wa kabila la mbilikimo ni wakazi asili wa kanda ya Afrika mashariki na kati, hadi sasa bado wanaishi kwenye maeneo ya misituni katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Afrika ya Kati, Burundi, Rwanda na Uganda.

    Zamani watu wa kabila la mbilikimo walipenda kujifunika mwili kwa majani ya mtende, na kujipamba kwa mifupa ya tembo, pembe za mbuzi na magamba ya kobe. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea vijiji vyao, wameanza kujifunza kuvaa nguo, lakini nguo zao zote walipewa na watalii.

    Mbilikimo wanawake wanajua kutengeneza vipodozi vya asili kwa kuchanganya juisi ya matunda yenye rangi mbalimbali na maziwa ya mama, na kuchora michoro ya mapambo usoni ili kurembesha nyuso zao na kujikinga na mashetani.

    Mbilikimo wanaume wote ni wawindaji hodari, wanatumia upinde waliotengeneza wenyewe kuwinda wanyama wakubwa kama tembo.

    Mbilikimo wanapenda sana kula mchwa, na wanaamini kuwa kula mchwa kunasaidia kujenga afya.

    Mbilikimo wanatunza sana misitu wanayotegemea kimaisha, na wanaruhusiwa kukata miti iliyokauka tu kwa ajili ya kupata kuni za kupikia. Inasemekana kwamba kulikuwa na timu moja ya wachunguzi iliyofika kwenye vijiji wanavyoishi mbilikimo, timu hiyo ilikata ovyo matawi ya miti, vitendo ambavyo viliwakasirisha wanavijiji wa huko na hatimaye timu hiyo ikafukuzwa kwenye eneo hilo.

    Ni kundi la watu wenye desturi za kipekee barani Afrika, lakini hivi sasa kabila la mbilikimo liko hatarini. Kabila la Bayaka ni kabila kubwa zaidi la mbilikimo nchini Cameroon, hivi sasa kabila hilo lina watu wasiozidi elfu 40, makabila mengine mawili yanayofuata kwa ukubwa yana watu 3,700 na 1000. Serikali ya Cameroon inachukua hatua kuhifadhi kabila la mbilikimo linalokabiliwa na hatari ya kutoweka.

    Mbali ya juhudi zinazofanywa na serikali ya Cameroon, masuala ya kuboresha maisha ya mbilikimo na kuhifadhi kabila hilo maalumu pia yamefuatiliwa na mashirika ya kimataifa. Baadhi ya nchi zimetekeleza sera maalumu kwa mbilikimo wanaoishi katika nchi hizo, zikiwahamasisha waondoke misituni na kuishi kama watu wa kawaida. Kutokana na kuongezeka kwa mawasiliano na jamii ya nje, ustaarabu wa kisasa umeleta mabadiliko kwa kabila hilo, na wameanza kuvaa nguo na kutumia vitu vya kisasa kama vile sabuni, kiberiti na sigara.

    Ingawa hali iko hivyo, watu wengi wa kabila la mbilikimo bado wanapendelea kuishi maisha ya jadi misituni kama walivyokuwa mababu zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako