• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aksu yajitahidi kujenga umaarfu wa chapa cha kilimo

    (GMT+08:00) 2015-07-01 16:23:39

    Aksu ni mji muhimu ulioko kusini mwa mkoa unaojiendesha wa kabila la Uighur wa Xinjiang, ambao ulikuwa ni kituo muhimu kwenye Njia ya Hariri ya kale. Waandishi wa habari wa Radio China Kimataifa hivi karibuni walitembelea mji huo na kugundua kuwa, katika mji huo ulioko kando ya jangwa la Taklimakan, watu wa huko wanalima mashamba ya miti ya matunda yenye eneo la zaidi ya kilomita 667 za mraba, na kilimo cha matunda kimekuwa chanzo kikubwa zaidi cha mapato ya wakulima wa huko. Wakati huo huo, serikali ya huko inahimiza kuendesha kilimo kutokana na mahitaji ya soko, na kujitahidi kujenga umaarufu wa chapa ya kilimo cha Aksu, jambo ambalo limewaletea wakulima wa huko manufaa makubwa ya kiuchumi.

    Hivi sasa wachina wanapoitaja Aksu, wengi hufikiria tufaha tamu sana. Tufaha bora za Aksu zinazalishwa kwenye mashamba ya Hongqipo. Kwa miaka kumi kadhaa iliyopita, Hongqipo ilikuwa bado ni jangwa, lakini hivi sasa imekuwa ni mashamba ya matunda yenye eneo la zaidi ya kilomita 133 za mraba. Kwenye mashamba hayo, waandishi wetu walikutana na Bw. Gu Long na mkewe ambao ni wakulima wa matunda kwenye mashamba hayo na wameishi kwenye Hongqipo kwa miaka zaidi ya kumi. Mke wa Bw. Gu Long alipokumbuka hali ya huko ilivyokuwa zamani wakati walipowasili Hongqipo anasema,

    "Kwa kweli, wakati ule sisi tulikuwa ni maskini sana, na tuliishi maisha magumu."

    Baada ya jitihada kwa zaidi ya miaka kumi, wanandoa hao wameanza kupata faida kubwa kutokana na shamba lao la matunda, na maisha yao yamekuwa mazuri zaidi kuliko wakati walipowasili Hongqipo. Mke wa Gu Long anasema,

    "Hivi sasa maisha yetu ni mazuri. Maofisa wa mashamba ya Hongqipo wanakuja hapa mara kwa mara na kutuelekeza kuhusu uzalishaji na kutujali hali ya maisha yetu. Sera ni nzuri, na maisha yetu yamekuwa mazuri kuliko zamani, miti ya matunda imekuwa mikubwa na kilimo cha tufaha kimeanza kuleta faida. "

    Bw. Gu Long amewaambia waandishi wetu kuwa, kama mahitaji ya soko ni makubwa, uzalishaji shambani unaweza kuleta pato la yuan zaidi ya laki mbili kwa mwaka, hata kama mauzo ya tufaha si mazuri, bado wanaweza kupata zaidi ya yuan laki moja kila mwaka.

    Kwenye mashamba ya Hongqipo, kuna familia elfu moja hivi zinazojishughulisha na kilimo cha matunda kama familia ya Gu Long. Mkurugenzi wa idara ya uzalishaji wa kilimo ya mashamba ya Hongqipo Bw. Xiong Yong amesema, Gu Long anapanda aina mbalimbali za matunda, kama angepanda tufaha tu, atapata faida kubwa zaidi. Shamba lenye eneo la mita zaidi ya 1300 za mraba linaweza kuleta faida ya Yuan laki saba hadi nane kwa mwaka. Kutokana na ladha nzuri, tufaha zinazozalishwa kwenye mashamba ya Hongqipo zinapendwa sana sokoni, kila mwaka wafanyabiashara wanakwenda Hongqipo kuagiza tufaha kutoka kwa wakulima, hivyo hawana wasiwasi wa soko. Bw. Xiong Yong anasema,

    "Kila mwaka wafanyabiashara wengi wanakuja hapa, na matunda ya hapa hata hayawezi kukidhi mahitaji makubwa ya soko. Kila mwezi Julai, wafanyabiashara huja kuagiza matunda kutoka wakulima. Kwanza wanalipa dhamana, na baada ya kupevuka kwa matunda, watalipa malipo yote kwa mujibu wa bei ya wakati ule sokoni. "

    Mazingiria maalumu ya kijiografia ya huko na mfumo wa usimamizi ni sababu muhimu ya sifa ya tufaha zinazozalishwa Hongqipo. Mbali na hayo, jitihada za serikali ya huko katika kujenga umaarufu wa chapa pia ni sababu nyingine muhimu. Bw. Xiong Yong anasema, katika miaka ya 90 karne iliyopita, tufaha za Aksu zilikuwa hazijulikani sokoni. Mashamba ya Hongqipo yalianza kueneza chapa yake, na kufungua soko hatua kwa hatua. Hivi sasa chapa ya Aksu inakubalika sana sokoni. Bw. Xiong Yong anasema,

    "Kila mwaka tunakwenda sehemu mbalimbali pamoja na tufaha zetu na kushiriki kwenye maonesho au mashindano. Tumepata uthibitisho mbalimbali wa sifa za bidhaa zetu kama vile ule wa vyakula vya kikaboni, Kama tukikamilisha mfumo wetu wa kimsingi, wataja wataweza tu kushughulikia vizuri zaidi biashara zao kwa kupitia jukwaa letu. Baada ya juhudi za miaka kadhaa, hivi sasa chapa yetu inajulikana siku hadi siku, na hatuna wasiwasi hata kidogo kuhusu soko la tufaha zetu."

    Shamba la miwalnut la wilaya ya Wensu ni kampuni kubwa mjini Aksu, na walnut zenye ngozi nyepesi zinazozalishwa kwenye shamba hilo zinajulikana sana sokoni. Tofauti na hatua ya kuvutia wateja inayofanywa na mashamba ya Hongqipo, shamba la Wensu linafuata utaratibu wa kuagiza, kusindikiza na kuuza mazao yao kwa pamoja. Hii si kama tu imeondoa wasiwasi wa wakulima kuhusu soko la mazao, bali pia inaweza kuongeza thamani ya chapa. Mkurugenzi wa shamba hilo Bw. Li Jie amewaambia waandishi wetu kuwa, shamba hilo lina wakulima 2700 hivi, na mwaka jana mapato ya wastani kwa kila mtu yalifikia yuan elfu 30. Anasema,

    "Wakulima wanashughulikia upandaji tu, walnut zetu zote ni za kikaboni, baadaye tunazikusanya, kushughulikia na kuuza kwa pamoja. Tunaziagiza kwa bei ya yuan 40 kilo moja, baada ya kushuguhlikiwa zinaweza kuuzwa kwa yuan 60 hadi 80 kilo moja."

    Mashamba ya Hongqipo na shamba la Wensu ni mifano miwili tu ya jinsi Aksu inavyojitahidi kujenga sifa ya kilimo chake. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya maendeleo ya kilimo ya idara ya kilimo ya Aksu Bw. Qing Cuishan amesema, hivi sasa Aksu inafanya juhudi kueneza utaratibu wa kuhamasisha kampuni kubwa ziagize mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima, ili kupunguza hatari ya soko kwa wakulima. Anasema,

    "Hivi sasa tumeanza kueneza utaratibu wa kuhamasisha kampuni kubwa ziagize mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima, ili kuunganisha maslahi ya kampuni na wakulima na hivyo kupunguza hatari ya sokoni kutokana na kuyumbayumba kwa bei, na hatimaye kuwanufaisha wakulima."

    Baada ya jitihada za miaka mingi, Aksu imepata mafaniko makubwa katika maendeleo ya kilimo na ujenzi wa chapa za kilimo. Hivi sasa kuna kampuni 748 za kilimo, ambazo zinahusisha na kunufaisha wakulima laki 2.3. Mji wa kale wa Aksu unaonesha uhai mpya katika ujenzi wa Ukanda wa uchumi wa Njia ya Hariri.

    Baada ya kusikia kuhusu mashamba ya Hongqipo na shamba la Wensu, hebu sasa tumzungumzie mkulima mmoja wa zabibu. Bw. Zhou Jun ni mkulima anayeishi Turpan, mkoani Xinjiang nchini China. Turpan inajulikana sana hapa China kutokana na zabibu zake, na Zhou Jun ndio mkulima anayepanda zabibu. Kutokana na jitihada zake, Bw. Zhou Jun anaishi maisha mazuri.

    Bw. Zhou ameendesha shamba lake la zabibu kwa miaka 9. Amemwambia mwandishi wetu kuwa, mwanzoni idadi ya zabibu alizopanda ilikuwa haiongezeki, pia alikuwa hawezi kuziuza kwa bei mwafaka. Miaka 9 iliyopita kutokana na msaada wa wakulima wengine, alianza kupanda zabibu za aina bora, na ameweza kupata faida mara tano kuliko zamani. Anasema,

    "Zamani baada ya kuuza zabibu nilipata yuan elfu 12 hivi, lakini hivi sasa naweza kupata yuan elfu 80 hivi. Zamani nilipata faida elfu 6 tu nikiondoa gharama, lakini hivi sasa naweza kupata faida yuan elfu 70 baada ya kuondoa gharama ya yuan elfu 10. "

    Zhou Jun ameanza kupanda zabibu akiwa utotoni, na ufundi wake unasifiwa sana na wataalam wa kilimo cha zabibu. Kutokana na uhodari na mazingira maalumu ya kimaumbile ya Turpan, zabibu kavu za Zhou Jun zina sifa nzuri sana. Tarehe 20 mwezi Agosti ni siku ya kuvuna zabibu, baadhi ya wafanyabiashara wameagiza zabibu za Zhou Jun. ingawa Zhou Jun hana wasiwasi kuhusu mauzo ya zabibu, lakini wakati wingine analazimika kukabiliana na mabadiliko ya bei. Hii imemfanya Zhou Jun atambue kuwa, ili kuhakikisha faida, lazima azitengeneze vizuri zaidi na kuzalisha zabibu kavu bora. Anasema,

    "Zabibu zangu zina sifa nzuri. Baada ya kushughulikiwa vizuri, urefu wa zabibu kavu utafikia centimeter 3 hadi 4, ambazo zinauzwa kwa bei kubwa. Watu hawana wasiwasi kuhusu bei, wana wasiwasi kuhusu ubora wa mazao."

    Ingawa Zhou Jun anapata faida kubwa, lakini analazimika kukabiliana na wanunuzi moja kwa moja, hii inaweza kuongeza hatari ya wakulima. Hivyo Zhou Jun ana matumaini kuwa shirikisho la ushirikiano wa wakulima linaweza kuwasaidia wakulima kupunguza hatari na kuzalisha zabibu kavu bora. Lakini hivi sasa bado hakuna shirikisho kama hilo, Zhou Jun amesema kama shirikisho hilo likiundwa, atajiunga nalo, kwani zabibu zinaweza kuuzwa kwa bei kubwa zaidi kuliko sasa.

    Zhou Jun anaridhika na maisha ya hivi sasa, mradi uliotekelezwa na serikali ya Xinjiang kuhusu kuwatajirisha watu na kuboresha makazi yao umeboresha mazingira ya makazi ya wakulima wa huko. Anasema,

    "Nafurahia maisha ya sasa. Nina nyumba, gari, akiba ya pesa. Nyumba yangu ina mita 105 za mraba, kuna umeme na maji. Wanakijiji wote ni kama hivi, tuna nyumba hiyo, na nyumba za zamani shambani pia zinabaki."

    Zhou Jun pia amesema, hivi sasa wakulima wamepata bima za uzeeni na afya, anaona maisha yake yanahakikishwa. Zhou Jun pia amesema, kwenye kijiji chao mtu akipenda kufanya juhudi, ataishi vizuri, lakini watu wavivu hawawezi kuishi maisha mazuri. Anasema,

    "Naridhika sana na maisha ya sasa, kama watu wote wanaweza kuishi maisha kama hayo, nchi yetu itakuwa na nguvu kubwa zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako