• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaweka malengo mapya ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2015-07-01 18:20:14

    China imetoa ahadi mpya katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, ikiweka malengo mapya ya baada ya mwaka 2020 ambayo ni juhudi zake kubwa katika kukabiliana na changamoto hiyo ya duniani.

    China, ikiwa ni nchi kubwa duniani kwa kutoa hewa inayosababisha ongezeko la joto, imelenga kupunguza kwa asilimia 60 hadi 65 ifikapo mwaka 2030, utoaji wa gesi ya carbon dioxide kwa kila uniti ya pato la taifa GDP ikilinganishwa na kiasi cha mwaka 2005 kufuatia hatua zilizoamuliwa na China, ambazo ni mpango wa utekelezaji uliowasilishwa kwa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

    Naibu mkuu wa kituo cha utafiti wa kimkakati na uhusiano wa kimataifa cha China kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Zou Ji anasema,

    "Malengo ya China ni kuwa tunatakiwa kufanya utoaji wa gesi ya carbon dioxide ufikie kilele chake wakati wastani wa pato la taifa kwa kila mtu utakapofikia dola za kimarekani elfu 14 hadi 15 tu, ambapo kiwango cha utoaji wa gesi hiyo kwa kila mtu kinapaswa kuwa chini ya kiwango cha Umoja wa Ulaya na Marekani katika historia."

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya wataalam wa mabadiliko ya hali ya hewa He Jinakun amesema China inatakiwa kufanya juhudi kubwa zaidi kuliko nchi zilizoendelea, na mabadiliko makubwa pia yatatokea katika njia ya kujiendeleza kiuchumi.

    "Kutoongezeka kwa utoaji wa carbon dioxide kunamaanisha kuwa makaa ya mawe na mafuta pia havitaongezeka, na ongezeko litakuwepo katika umeme unaozalishwa kwa maji, upepo, nishati ya jua na umeme wa nyuklia. Ndiyo maana, kila mwaka China inapaswa kuzalisha upya umeme wa upepo wa kilowati milioni 20, umeme wa jua wa kilowati milioni 20 na umeme wa nyuklia wa kilowati milioni 10, ili kutimiza malengo hayo. Nchi yoyote iliyoendelea haina uwezo huu, na juhudi zitakazofanywa na China zitakuwa kubwa sana."

    Mpango huo unaelekeza kuwa, ili kufanikisha malengo, China itayaunga mkono maeneo 15 ikiwemo mkakati wa kitaifa, mkakati wa kikanda, utaratibu wa nishati, mtaji, na uhusiano wa kimataifa. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Zhang Yong ameeleza kuwa hivi sasa China inakamilisha sera na hatua kwa mujibu wa mpango wa mkakati wa kitaifa kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    "China inafanya majaribio katika mikoa sita na miji 36 kote nchini ili kutafuta njia za ufanisi za kufanya utoaji wa carbon dioxide ufikie kilele chake. China inajitahidi kujenga miundombinu, na imetangaza orodha ya miradi inayopewa kipaumbele na taifa inayosaidia kupunguza utoaji wa carbon dioxide, kuzidisha ukusanyaji na data zinazohusu hewa zinazosababisha ongezeko la joto, kuendeleza kazi za kubadilisha taarifa kuhusu hewa hizo kati ya nchi zinazoshiriki kwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, kuanzisha siku ya taifa ya kiwango cha chini cha carbon dioxide, na pia kuongeza matangazo ya elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo ya kiwango cha chini cha carbon dioxide."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako