• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ugonjwa wa Simu

    (GMT+08:00) 2015-07-02 10:51:18

    Kwa sasa matumizi ya internet kwa njia ya simu ni jambo lililozoeleka karibu katika miji mingi ya Afrika. Hapa China matumizi ya internet kwa njia ya simu yanaendelea kubadilika kila kukicha, na sasa imefikia kasi kuwa watu wana uraibu wa internet na wengine ni kama hawezi hata kuacha simu zao. Katika kipindi chetu tuliweka masuali kwa wasikilizaji wetu kama mambo nitakayotaja yanawagusa? Kwanza, kama umeacha simu nyumbani, huwezi kutulia na kufanya kazi kwa makini? Pili, kama simu yako iko kimya kwa muda mrefu, utaichukua na kuangalia kama imeharibika au imezima? Tatu, una hisia za simu kuita hata kama haiiti, au unasikia milio ya simu za wengine, lakini unaona ni yako? Nne, unaogopa simu yako itazima kutokana na kutokuwa na chaji. Tano, kama simu yako haiwezi kuunganishwa na Internet, utakasirika au la? Kwa undani zaidi hebu kusikiliza kipindi chetu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako