• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya kibiashara ya China kukamilika hivi leo jijini Nairobi nchini Kenya, huku makampuni yakitangaza mafanikio makubwa.

    (GMT+08:00) 2015-07-03 10:16:13

    Maonyesho ya kibiashara ya China jijini Nairobi nchini Kenya yanatarajiwa kukamilika hivi leo Ijumaa, huku makampuni ya Kichina yakitangaza mafanikio makubwa katika maonyesho hayo ambayo yamechukua siku tano tangu Jumatatu.

    Maonyesho hayo ambayo uandaliwa kila mwaka na ambayo yamevutia zaidi ya makampuni 250 ya kutoka nchini China mwaka huu, yametangazwa na makampuni kuwa na mafanikio makubwa.

    Hii ni baada ya kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wateja na makampuni hayo kupata vianzo vingi vya mauzo ya bidhaa zao, pamoja na kuwapa habari wateja wapya pamoja na kuendelea kutunza wale wa zamani.

    Wang Liu ni mkurugenzi wa mkuu wa kampuni moja ya kuunda fanicha kutoka nchini China, na anasema maonyesho haya ya mwaka huu yamekuwa ya fanaka kuliko mwaka jana kwa kuwa amepata nafasi ya kuonyesha bidhaa zake.

    Radio China Kimataifa imepata nafasi ya kuingia katika kibanda chake.

    "Katika maonyesho haya nimepata nafasi ya kuonyesha bidhaa zangu za fanicha kwa wateja, na natumahi wakenya zaidi watapata nafasi nzuri ya kuona bidhaa hizi.Fanicha hizi tunaunda hapa nchini Kenya lakini tunaagiza mali ghafi kutoka nchini China na kuunda na wafanyikazi wa humu nchini na tumefanya kazi hii kwa zaidi ya miaka mitatu sasa."

    Kando na kibanda cha kampuni ya Bwana Liu, pia Radio China imetembelea kibanda kingine cha kampuni ya uundaji magari, cha Jiangui.

    Fidelis Osiemo ni afisa mkuu wa mauzo katika kampuni hii ya kutoka China.

    "Haya magari niyakutoka nchini China, kutoka kampuni ya Jiangui na yamependwa na watu wengi humu nchini. Mashule, makampuni ya uchukuzi na pia makampuni ya usafiri wa umma yamependa magari haya, tunasema hakika maonyesha haya yamekuwa na mafanikio. Magari haya yanga ingini zilzona nguvu sana na yanatumia mafuta vizuri."

    Maonyesho haya yamekuwa yakiandaliwa kila mwaka hapa jijini Nairobi, na waandalizi wake wanasema huenda hivi karibuni wakaanza pia kuyaandaa katika miji ya Mombasa na Kisumu, ili kuweza kuwafikia wateja wengi iwezekanavyo.

    Upanuzi wake unawadia wakati ambapo Biashara kati ya China na mataifa ya Afrika, inaendelea kuongezeka na ni katika njia hii pekee ambapo Biashara itaweza kunawiri zaidi.

    Kando na makampuni hayo mawili pia katika maonyesho haya, kuna makampuni mengine kama yale ya kutengeneza vyombo vya kurushia matangazo ya radio na runginga, makampuni ya kuunda piki piki miongoni mwa makampuni mengine.

    Pia wanabiashara wa Afrika wamefika katika maonyesho haya, na Bwana Abdul Mohamed ni mmoja wao.

    Amekuwa akifanya Biashara kati ya China na Afrika, na amefika hapa kuitangaza kampuni yake ya usafirishaji wa bidhaa kutoka China hadi Afrika.

    Anasema Biashara ni nzuri japo amekuwa na shida ya lugha, pamoja na wafanyibiashara wengine kutoka Afrika ,ambao ufanya Biashara kwa wingi na China.

    Sasa anasema wafanyabiashara wanafaa kuchangamkia lugha tofauti tofauti, ili waweze kufanya Biashara kila mahala Ulimwenguni.

    "Tatizo la lugha ndiyo shida yetu kubwa, kwa hivyo itakuwa muhimu kwa wachina kujifunza kiingereza na sisi tujifunze kichina ili tuweze kufanya Biashara vuzuri."

    Maonyesho ya mwaka huu yakikamilika hivi leo, makala ya mwaka huu yatatumika kama nguvu mpya, za kuendelea kuimarisha Biashara na ushirikiano wa kiuchumi, kati ya China na Afrika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako