• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atembelea mradi wa ushirkiano wa usafiri wa anga kati ya China na Ufaransa

    (GMT+08:00) 2015-07-03 19:17:28

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, aliyepo ziarani nchini Ufaransa, akiwa na mwenzake Manuel Valls wa Ufaransa wametembelea mradi wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika makao makuu ya kampuni ya Air-Bus mjini Toulouse.

    Mawaziri hao wameshuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya kuanzisha kituo cha kukamilisha na kukabidhi ndege ya aina ya A-330 mjini Tianjing, China ambacho kitakuwa ni mradi wa kwanza wa ndege kubwa wa kampuni hiyo nje ya Ulaya.

    Akiutaja ushirikiano wa usafiri wa anga kati ya pande hizo mbili kuwa mfano wa kuigwa, Bw. Li amesema ushirikiano huo sio uhusiano kati ya mteja na mwuzaji tu, bali ni muingiliano wa kimkakati wa nguvu za kila upande.

    Katika ziara hiyo ya Li Keqiang, China na Ufaransa pia zimekubaliana kushirikiana kuendeleza soko la upande wa tatu kwa pamoja ili kupata manufaa kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako