• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misaada ya masomo ya China inakuza uchumi na jamii Nigeria

    (GMT+08:00) 2015-07-04 19:25:20






    Msaada wa udhamini wa masomo unaotolewa na China kwa wanafunzi wa Afrika unasaidia kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii barani humo. Hayo ni kwa mujibu wa gavana wa Jimbo la Kano aliyetembelea wanafunzi kutoka jimbo lake wanaosemea katika vyuo mbalimbali hapa nchini China kwa msaada wa China.

    Gavana wa Jimbo la Kano, Dkt. Rabiu Musa Kwankwaso kwenye ziara yake ya barani Asia kwanza alifika hapa Beijing, na kuwatembelea wanafunzi kutoka kwenye jimbo lake. Lengo la kukutana na wanafunzi hao lilikuwa ni kubadilishana nao maoni kuhusu uzoefu waliopata vyuoni, na kufanya mazungumzo na maofisa wa China kuhusu uwezekano wa kuongeza udhamini zaidi kwa wanafunzi wa Afrika hususan Nigeria, ili kuhimiza maendeleo ya uchumi.Alisema.

    "Wanafunzi wengi wanaohitimu wanaajiriwa, sio Nigeria tu bali pia kwenye nchi mbalimbali na wengine katika serikali ya jimbo la Kano na kwenye vyuo. Sijasikia malalamiko yoyote kuhusu wanafunzi wa Nigeria walioko hapa China, na naweza kusema uhusiano wa China na Nigeria katika sekta ya elimu ni mzuri. Naamini kwamba kwao kuja hapa china kutawasaidia wao wenyewe, jamii zao nan chi yetu kwa jumla"

    Mwaka huu zaidi ya wanfunzi 100 wa Nigeria, walipata msaada wa masomo kutoka kwa serikali ya China na hamsini kati yao ni kutoka jimbo la Kano.

    Sulaiman Mu'azu anazomea Chuo cha Liaoning

    "Matarajio yangu ni kupata matokeo mazuri niwezavyo, kwenye taaluma ninayosomea na kurejea katika jimbo langu kutoa mchango wa maendeleo"

    Mojawepo wa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Afrika wanaosomea hapa Beijing ni lugha.

    Lakini ili kutatua tatizo hilo, serikali ya China kwa ushirikiano na zile za Afrika zimeanzisha taasisi mbalimbali za Confucius kutoa mafunzo ya Kichina.

    Katika jimbo la Kano kuna taasisi moja ya kutoka mafunzo ya lugha na tamaduni za kichina.

    Mukhtara Rosani amekuwa akijifunza kichina nchini Nigeria na ameandama na gavana kwenye ziara hii. Yeye na wenzake 22 watasalia China kwa miezi mitatu kujifunza zaidi lugha na kutembelea maeneo mbalimbali

    "Jana tulitembelea tian an men square na leo tulikuwa kwenye ukuta mkuu. Jana tulipoenda sokoni tuliweza kujadili bei bila wasi wasi kwa sababu tunafahamu kichina. Na tunajua kusema ah hii ni ghali mno……kwa hivyo naona hii lugha ni muhimu sana kwa sababu kuna wachina wengine katika jimbo la Kano na tutawafunza wafanyibiashara wetu kuongea kichina."

    Kwa sasa serikali ya jimbo la Kano imetoa mafunzo ya lugha ya kichina kwa waalimu wenyeji ambao wataanza kufunza lugha hiyo katika shule zao.

    Mafunzo hayo yana manufaa hata kwa wasiokuwa na lengo la kwenda kwa masomo zaidi nchini China kwa sababu.

    "kuna wachina wengi wanaofanya biashara katika jimbo la Kano, na pia kuna viwando kadhaa vya wachina kwenye jimbo hilo, na hivi karibuni kampuni moja ya China ilinunua ekari 41 za ardhi na nyumba 286 kwa gharama ya zaidi ya naira bilioni 5 zote hizo ziko kwenye mji wa amana ambao tulianzisha miaka 3 iliopita "

    Kulingana na Gavana Musa, idadi ya wanafunzi wa Nigeria wanaopata udhamini wa masomo kuja hapa nchini China inatarajiwa kuongezeka na kunufaisha wengi waliofuzu lakini hawana fedha za kuendelea na masomo ya juu.

    Hata hivyo mamia ya wengine hujiunga na vyuo mbalimbali vya China kama wanafunzi wa kujitegemea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako