• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa China na Afrika kwenye sekta ya habari ni muhimu

    (GMT+08:00) 2015-07-04 19:27:59






    Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014, hivi sasa thamani ya biashara kati ya China na Afrika ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni 200. Pamoja na kuwa thamani hiyo inatokana na ushirikiano wa kibiashara, na ushirikiano kwenye ujenzi wa miundo mbinu na teknolojia, kumekuwa na maendeleo pia kwenye ushirikiano katika sekta za utamaduni na sekta ya habari. Sekta ya habari imekuwa ni moja ya maeneo muhimu ambao yanafursa nyingi za ushirikiano, hasa ikzingatiwa kuwa China na Afrika zimekuwa wahanga wa propaganda za vyombo vya habari vya magharibi.

    Ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabikana na hali hiyo, mwaka jana China ilianzisha kituo cha kupanua uwezo wa vyombo vya habari vya China na Afrika kutangaza zaidi maswala yenye umuhimu kwa pande zote mbili, kama anavyoeleza Jacob Mogoa

    Mapema mwaka huu jumla ya watu 17 waliuawa nchini Ufaransa katika shambulizi la kigaidi kwenye ofisi za jarida moja la vibonzo nchini Ufaransa. Vyombo vikubwa vya habari vya nchi za magharibi vilifuatilia kwa karibu wiki nzima tukio hilo, ambalo pia liliwafanya viongozi mbalimbali duniani kufanya maandamano katika mji mkuu Paris. Lakini wakati huo huo Afrika magharibi nchini Nigeria, kulikuwa na tukio la zaidi ya watu 2, 000 kuuawa baada ya kushambuliwa na kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo. Licha ya mauaji hayo, vyombo vya habari vya magharibi havitangaza tukio hilo kwa uzito licha ya kuwa na idadi kubwa ya wahanga.

    Evans Muhando ambaye ni mwanahabari wa Tanzania anayesoma nchini China, anasema kuna mambo mengi yanayochangia hali hiyo katika nchi zinazoendelea hususan barani Afrika.

    Katika juhudi za kuendeleza uhusiano kwenye sekta ya habari, mwaka jana China ilianzisha kituo cha ushirikiano wa mambo ya habari kati yake na Afrika,.

    Kituo hicho kilianza kutoa mafunzo ya kwanza kwa waandishi wa habari wa Afrika yanayolenga kuinua ufahamu wa waafrika kuhusu China. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw Qin Gang anasema kituo hicho kitawafanya waafrika kupata maelezo kamili kuhusu China kinyume na wanazopata kutoka kwa vyombo vya habari vya magharibi.

    Baada ya kushuhudia ripoti zisozofaa kuhusu China ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari vya magharibi, mwandishi wa gazeti la kila siku la Tanzania Daily News Bw Abduel Elinaza aliamua kuwa miongoni mwa kundi la kwanza kutoka Afrika kuhudhuria mafunzo ya miezi kumi ya kuielewa zaidi China. Elianaza anasema kinyume na inavyoripotiwa, China ni nchi ambayo inazitakia mema nchi za Afrika.

    Katika pita pita zetu mitaani nchini China, tuligundua kuwa ni wachina wachache ambao wanaufahamu zaidi kuhusu waafrika na bara la Afrika kwa ujumla. Hata hivyo mratibu wa kituo hicho cha ushirikiano wa habari kati ya China na Afrika Bibi Xiaomei Zhou anasema kupitia waandishi wa China waliohudhuria mafunzo hayo wamejifunza mengi kuhusu bara la Afrika.

    Vyombo vingi vya habari barani Afrika kwa muda mrefu vimekuwa vikikumbwa na changamoto kubwa katika kutekeleza majukumu yao kutokana na ukosefu wa teknolojia ya kisasa ya upashanaji habari. Hata hivyo Bw Evans Mhando anasema njia pekee ya vyombo vya habari vya Afrika kushindana kikamilifu na vile vya Magharibi ni kukumbatia teknolojia ya kisasa ya uanahabari.

    Tofauti kabisa na matarajio ya wengi, waafrika wamekuwa wakiifahamu China kama nchi ya watu wanaofahamu tu mchezo wa kungfu. Hata hivyo hivi sasa ambapo waaandishi wa habari wa Afrika wanaendelea kuizuru nchi hii kuna matumaini makubwa kuwa mtazamo wa China barani Afrika utaendelea kubadilika na watu wa pande zote mbili watafanya mawasiliano zaidi ambayo yatasaidia kuhimiza maelewano na ushirikiano wa pande zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako