• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Russia wafanya mazungumzo ya simu

    (GMT+08:00) 2015-07-05 19:36:19

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang tarehe 3 alasiri aliongea kwa simu na waziri mkuu wa Russia Dmitry Medvedev.

    Bw. Medvedev amesifu uhusiano kati ya Russia na China. Amesema kuwa anatarajia kufanya ziara nchini China na kuhudhuria mkutano wa 12 wa mawaziri wakuu wa China na Russia kabla ya mwishoni mwa mwaka huu na kuutakia mafanikio mkutano huo.

    Bw. Li Keqiang amesema utaratibu wa mawaziri wa China na Russia kukutana kila baada ya muda fulani una ufanisi, China inapenda kushirikiana na Russia kuandaa vizuri mkutano ujao, na kuhimiza uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili upate maendeleo mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako