• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto wa shule nchini Kenya wawaokoa wasichana na ubakaji baada ya kufundishwa kauli "NO MEANS NO"

    (GMT+08:00) 2015-07-06 08:59:54

    Tuliwahi kuzungumzia suala la ubakaji na madhara yake kwa wasichana na wanawake. Kwa kuzingatia hali ya sasa ilivyo na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji, serikali ya Kenya imeanzisha kampeni ya "NO MEANS NO" maana yake, HAPANA MAANA YAKE NI HAPANA. Kampeni hii inatoa elimu kwa vijana wa kike na kiume kuhusu kupambana na vitendo viovu katika jamii.

    Kampeni kama hiyo inatakiwa kuanzishwa katika kila nchi, zinazoendelea na zilizoendelea, maana vitendo vya ubakaji au unyanyasaji wa kijinsia vinatokea sehemu zote. Nchini Kenya, mwanafunzi mmoja alipokuwa njiani kuelekea shule, alimwona mwanaume mmoja akijaribu kumvua chupi mtoto wa kike huku akienda naye kando ya mto. Kijana huyo akihisi kuwa mtu huyo alikuwa na nia ya kumbaka mtoto, na kutokana na mafunzo aliyopata kuhusu kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ubakaji, aliwaita vijana wenye umri mkubwa ambao walimsaidia kukabiliana na mwanaume huyo na hivyo kumwokoa mtoto wa kike aliyekuwa kwenye hatari ya kubakwa.

    Ukijaribu kufikiri, bila ya mafunzo aliyopata kijana huyo, mtoto huyo wa kike angepona kweli? Collins Omondi, ambaye amemfundisha kijana elimu hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake anasema, mtoto huyo asingepona, kwani kama mtu huyo angefanikiwa kumbaka, angemtupia mtoni, maana alikuwa akimvuta kuelekea ukingoni mwa mto. Omondi anafundisha kwenye mradi unaoitwa "Wakati wao wa Ukweli" ambao unasimamiwa na shirika la kujitolea la Ujamaa Afrika. Mradi huo unawafundisha vijana kupambana na uhalifu dhidi ya wanawake.

    Katika shule ambazo kampeni hii imefanyika, vitendo vya kubughudhi watoto wa kike vimepingua, na pia vitendo vya kubakwa na marafiki wa kiume na marafiki vimepungua kwa asilimia 20, kutoka asilimia 61. Omondi anasema, lengo hasa la kufundisha somo hilo ni kuwa na vijana wenye tabia nzuri, uwezo, na kuwa waadilifu kwenye masuala yanayohusiana na kuzuia ubakaji na kusimamia haki za wanawake.

    Hebu sasa tugeukie hapa China na tunaangalia kesi moja ya ubakaji iliyotokea mwaka 2013. Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 tu katika mkoa wa Guang Xi, kusini magharibi mwa China anayeitwa Xiao Yu alibakwa na wazee watatu kwa mara nyingi. Mzee mmoja alikuwa na miaka 74, mwingine 60, na wa tatu 72. Mwanzoni Xiao Yu alikuwa anaogopa sana, akaamua kutowaambia wazazi wao kuhusu balaa lake. Lakini mzazi ni lazima utagundua kuwa mtoto wako hayuko vizuri, kuna kitu kinamsumbua. Hivyo baada ya muda mrefu, alimwambia baba yake. Yafuatano ni mahojiano kati yake na mwandishi wa habari:

    "Baba yako alikuuliza kwa njia gani?"

    "Aliponipiga mara ya mwisho, aliniuliza, nikamwambia."

    "Kabla ya hapo, hukumwambia?"

    "Sikumwambia."

    "Uliogopa nini?"

    "Niliogopa kuwaambia jambo hilo."

    "Baba yako ameniambia kuwa watu hao walikutishia. Walikutishia vipi?"

    "Walichukua kisu, na kutaka kuniharibu kwa kucha zao."

    "Kwa nini baada ya jambo hilo kutokea, hukuwaambia wazazi wako?"

    "Wale watu waliniambia nisiseme, nikisema wataniua."

    Tishio kama hilo hutolewa kwa watoto/wanawake/hata watoto wa kiume pale wahalifu wanapowafanyia kitendo hicho kiovu. Ni muhimu sasa kwa mzazi kuwa karibu na mtoto kwani kutamrahisishia kukueleza tatizo analokumbana nalo. Kwa upande wa baba yake Xiaon Yu, aliwaza nini mara baada ya kuambiwa kadhia iliyokuwa inamkabili mtoto wake?

    "Niliwaza njia nitakayotumia kuwaua watu hao. Nilifikiri kwa siku kadhaa, nikampigia simu kaka yangu. Namwambia, 'kaka, kama kitu chochote kikinitokea, uitunze familia yangu.' Lakini kaka alinishwishi nisifanye jambo hilo la kijinga, ananifikiria sana."

    Kusema kweli hilo ndilo jambo la kwanza ambalo mtu atafikiria. Maana ukiwaza mateso ambayo mtoto wako ameyapata, hasira ni kali mno, na unaona kama kuna kitu kitakachopunguza hasira hiyo ni kuwafutilia mbali watu hao. Msemaji wa Mahakama Kuu ya China Sun Jungong alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na vitendo vya ubakaji dhidi ya watoto wa kike.

    "Kanuni yetu ni kutovumilia vitendo vya ubakaji dhidi ya wasichana, na kuwalinda kadiri tunavyoweza. Ni lazima tulinde maslahi ya haki ya watoto wadogo, wasiharibiwe kutokana na vitendo vya uhalifu, na wawe na mazingira mazuri yenye afya, utulivu. "

    Kama alivyosema Sun, ni vema kulinda haki za watoto wadogo, wa kike na kiume, maana vitendo vya ubakaji wanafanyiwa watoto wa jinsia zote. Tuwalinde watoto wetu ili waweze kuwa raia wema hapo baadaye. Maana kama wasiposaidiwa wakati wakiwa wadogo, na wao wanaweza kuwafanyia wengine kitendo hicho cha kidhalimu. Xu Kai ni mtangazaji, na ana haya ya kusema

    "Shule zinapaswa kuwaelimisha wanafunzi ujuzi husika tangu siku ya kwanza ya masomo. Na kwa wazazi, kabla ya watoto wao kwenda shule, wakati wanapoanza kufahamu mambo ya jamii, wanatakiwa kuwaelezea jambo hili. Kama vile sehemu gani za mwili zao ni nyeti, ni binafsi, na ni marufuku kuguswa na wengine, kuguswa namna gani kuna dhamira mbaya, na mambo kama hayo, wazazi wanatakiwa kuwaelimisha watoto wao"

    Kipindi kimoja cha kuwaelimisha watoto nchini China kinaeleza sehemu za mwili ambazo haziwezi kuguswa na wengine ovyo ovyo

    "Sehemu tunazovaa nguo za kuogelea, kifuani, mdomo, na sehemu ya katikati ya miguu, zisiguswe na wengine ovyo. Tunapaswa kujua miili yetu, na kuusimamia. Kama wengine wanataka kugusa mwili wako, unatakiwa ukatae kwa nguvu. Usikubali wakushike mwili wako kutokana na maneno yao ya kubembeleza. Na pia hatuwezi kuvamia mwili wa mtu mwingine vilevile."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako