• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la 6 la opera ya Nanluoguxiang

    (GMT+08:00) 2015-07-06 10:30:54

    Karibu katika kipindi cha utamaduni wetu. Kufuatia ongezeko la ushirikiano kati ya China na Afrika, waafrika wengi wanakuja hapa China kufanya biashara au kutafuta ajira, Bibi Candice Botha kutoka Afrika Kusini pia ni mmoja wao. Lakini tofauti na wengine, Bibi Botha akiwa na mapenzi makubwa ya muziki, anajitafutia kazi ya kufundisha muziki katika shule ya kimataifa jijini Shanghai, China. Mwandishi wetu wa habari Xie Yi anakufahamisha jinsi Candice anavyofundisha muziki hapa China. 


    "Nimeishi hapa Shanghai kwa miaka mitatu, na sasa nafundisha sanaa ya maonesho na kwaya katika shule ya kimataifa."

    "Nilikuja hapa China kwa sababu nilijua itakuwa changamoto kubwa, pia naongezea ukurasa mpya kwenye kitabu cha maisha yangu."

    Kazi ya ufundishaji ya Candice jijini Shanghai ilianza katika Disney English, na baada ya kujiimarisha katika mji huo kwa mwaka mmoja, alihamia katika Shule ya Kimataifa ya Shanghai Community, ambako alianza kufundisha sanaa ya maonesho na kwaya.

    "Baada ya kufundisha katika shule hiyo ya kimatiafa, nimepata uhusiano wa karibu zaidi na watoto hawa, kwa sababu nimewahi kuwa katika sehemu mbalimbali na nafahamu hasa jinsi mtu anavyohisia akiwa katika nchi ya kigeni na mji wa kigeni. Na kwa kweli nataka kuwafahamisha mambo ninayoyafahamu pamoja na uzoefu wangu."

    Kipaji cha muziki cha Candice na uzoefu wake katika maonesho ulianza tangu akiwa mtoto huko Afrika Kusini, ambapo alianza kupiga gitaa wakati akiwa na umri wa miaka 15 na kujiunga na bendi moja. Lakini anaona maendeleo yake kama mwanamuziki yalikwama huko nchini kwake.

    "Naona hakuna fursa nyingi sana nchini Afrika Kusini. Watu wanapenda mtindo mmoja tu, lakini kwa mfano barani Ulaya, watu wako wazi kwa kila kitu, hali kadhalika na hapa China. Nimepata maoni mengi mazuri kuhusu muziki wangu ambayo sijawahi kusikia huko nyuma."

    Kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo Ty Smeins, uzoefu wa Candice wa maonesho na ufudishaji nchini Afrika Kusini na hapa China unaonesha anafaa kufundisha sanaa ya maonesho na kwaya.

    "Tulikuwa tunatafuta mtu wa kuziba pengo, na mtu huyo lazima awe na ustadi mwingi tofauti. Na bahati nzuri aliweza kuziba pengo hilo na amefanya kazi nzuri zaidi kuliko tulivyotarajia. Hivyo yeye ni hodari sana."

    Kutokana na wanafunzi wengi wa Candice kuwa ni wazungumzaji wazawa wa Kiingereza, hivyo baadhi ya wakati masomo yanakuwa magumu kwa wanafunzi wa China akiwemo Romain.

    "Baadhi ya wanafunzi wa China kama mimi, wana tatizo la lugha ya Kiingereza. Kama ukitaka kushiriki kwenye sanaa ya maonesho, unatakiwa kuwa na kiwango kizuri cha lugha."

    Lakini, Candice ana imani kuwa darasa la sanaa ya maonesho linaweza kuwafanya wanafunzi wawe wazuri zaidi hata kwa wale wenye aibu zaidi, na pia anashauri lisambazwe kote nchini China.

    "Michezo inamsaidia kujisikia raha pamoja na marafiki zake. Anaweza kuongea na kujisikia raha akiwa nao pamoja. Nataraji kumwona akiondoa aibu yake hadi kufikia mwishoni mwa muhula huu."

    Ingawa ana hamu kubwa ya kufundisha, lakini Candice anapanga kuacha kazi yake hiyo na kuendelea na masomo yake ya muziki ili katika siku za baadaye aendeleze kazi yake ya kuonesha jukwaani, na pia ana ndoto kwamba siku moja ataweza kufungua ukumbi wake kwa ajili ya wasanii.

    "Nina ndoto ya kufungua duka la kahawa ambalo litakuwa kama kituo cha wasanii, ambacho wasanii wanaweza kuja na kuchora kwenye kuta, na wanamuziki wanaweza kuja na kufanya maonesho. Kila mwezi tutakuwa na wasanii na wanamuziki tofauti. Hii ni ndoto kubwa."

    Hivi karibuni tamasha la 6 la opera ya Nanluoguxiang limefanyika hapa Beijing. Nanluoguxiang ni eneo la makazi ya zamani kwenye kitovu cha Beijing, ambako kuna makazi ya mtindo wa jadi wa Beijing na vichochoro. Mchezaji dansi kutoka Cameroon Simon Abbe amealikwa kuja kutumbuiza katika tamasha hilo. Abbe na kundi lake la wachezaji dansi walifanya maonesho yanayoitwa "Uwezo unaosahaulika". Maonesho hayo yanalenga kuwakumbusha watu uwezo uliofichika ndani yao, na kuwaambia watu kuwa wasisahau uwezo wa kiasili katika jamii ya kisasa. Mwandishi wetu wa habari Ronald Mutie amepata fursa ya kwenda kushuhudia tamasha hilo na kumhoji Bw. Abbe, na hapa ametuandalia ripoti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako