• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muziki wa kidijitali barani Afrika

    (GMT+08:00) 2015-07-06 10:34:54

    Msikilizaji mpendwa, karibu katika kipindi cha utamaduni wetu. Kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, njia ya kusikiliza muziki imebadilika barani Afrika. Katika miaka ya 80 karne iliyopita, CD ilichukua nafasi ya tepu ya kurekodi sauti. Hadi sasa CD bado haijatoweka, ingawa Afrika imejiunga na mwendo wa kidijitali wa kupata muziki wake duniani.


    Sekta ya burudani mwishowe imetambua mapinduzi ya simu za mkononi na kufanya juhudi ya kutoa huduma mpya kwa kuwekeza wasanii wa huko barani Afrika katika mambo ya muziki.

    Mtendaji mkuu wa shirikisho la kimataifa la shughuli ya sahani ya santuri Fraces Moore hivi karibuni alisisitiza umuhimu wa Afrika unaozidi kuongezeka. Alisema, Afrika ni bara ambalo uchumi wake unakua haraka, na kuenea kwa teknolojia kunawezesha wanachama wa shirikisho hilo na wenzi wake wa biashara kupata wateja wengi wapya.

    Mwaka 2014, mapato ya muziki wa kidijitali ya sekta ya burudani duniani yaliongezeka kwa asilimia 6.9 hadi kufikia dola bilioni 6.85 za kimarekani. Mapato ya uuzaji wa muziki za kidijitali ni sawa na thamani ya uuzaji wa CDs.

    Mauzo ya CDs katika masoko makuu matatu ya Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Kenya na Nigeria, yanaonesha kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na upatikanaji wa muziki za kidijitali.

    Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2017 kiwango cha muziki wa kidijitali katika muziki wa kurekodiwa barani humo kitaongezeka hadi asilimia 67. Nchini Kenya, kwa mwaka huu matumizi ya muziki wa kidijitali yanatarajiwa kuzidi yale ya muziki wa CD.

    Lakini je, hali hiyo ya kuingia kidigitali imeleta maendeleo ama imezuia maendeleo hususan katika mataifa yanayoendelea?

    Mwandishi wetu Mark Muli ameandaa ripoti ifuatayo kuhusiana na swala hilo nchini Kenya.

    Mbali na hayo leo pia tumemwalika mwenzetu DJ Mosy ambaye yeye sio tu DJ wa redio yetu, bali pia yeye ni mtayarishaji wa muziki . Karibu DJ Mosy.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako