• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukusanya fedha ili kufufua soko la hisa

    (GMT+08:00) 2015-07-06 11:01:49

    Kamati ya usimamizi wa hisa ya China jana usiku ilisema, Kampuni ya Hisa ya China CSF itakusanya fedha kupitia njia mbalimbali na kupanua wigo wake wa biashara ili kusaidia soko la hisa kuwa "tulivu."

    Benki kuu ya China itaisaidia kampuni ya CSF kuwa na uwezo zaidi wa kubadilisha mali na kuwa pesa taslim.

    Hatua hizo za kuunga mkono zinachukuliwa ili kusaidia soko la hisa linalodidimia. Soko la hisa la Shanghai lilishuka thamani kwa asilimia 29 katika wiki tatu zilizopita, na asilimia 12 ilikuwa katika wiki iliyopita.

    Juzi kampuni 21 kubwa za biashara ya hisa za China zilitangaza kuwa zitatumia dola za kimarekani bilioni 19.62, au asilimia 15 za mali zao katika mifuko ya biashara ya hisa ya makampuni yenye faida kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako