• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China huhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS nchini Russia

    (GMT+08:00) 2015-07-06 19:38:56

    Wizara ya mambo ya nje ya China imefahamisha kuwa rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano wa kilele wa kundi la BRICS na Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai utakaofanyika nchini Russia. Naibu waziri wa mambo ya nje Bw. Cheng Guoping amesema, China inatarajia kuwa ushiriki wa rais Xi utahimiza ushirikiano kati ya nchi wanachama wa jumuiya hizo mbili na kuanzisha umoja wenye mustakbali na maslahi ya pamoja.

    Wiki hii, rais Xi Jinping wa China atakwenda Russia kuhudhuria mkutano wa saba wa wakuu wa nchi za BRICS utakaofanyika huko Ufa. Hii ni mara ya tatu kwa rais Xi kuhudhuria mkutano wa BRICS. Kuhusu ziara hiyo, naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Cheng Guoping amesema, hii inaonesha kuwa China inatilia maanani sana ushirikiano kati ya nchi za BRICS.

    "Wakuu watano wa nchi za BRICS watakutana na kubadilishana maoni kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo na masuala ya kimataifa na kikanda wanayofuatilia kwa pamoja. Makubaliano yatakayofikiwa yatatangazwa kwenye Azimio la Ufa litakalotolewa baada ya mkutano. Kwenye mkutano huo, viongozi hao pia watafanya mazungumzo na viongozi wa nchi wanachama na nchi waangalizi wa Jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai, Umoja wa kiuchumi wa Ulaya na Asia, na viongozi wengine wa nchi zilizoalikwa na wakurugenzi wa mashiriki ya kimataifa. Aidha, viongozi hao pia watafanya mazungumzo na wawakilishi wa Baraza la biashara na viwanda la nchi za BRICS."

    Hivi sasa nchi wanachama wa BRICS zimezidisha ushirikiano kati yao na kuimarisha uratibu na mawasiliano kuhusu masuala muhimu ya kimataifa, hali ambayo imelifanya kundi hilo liwe nguvu muhimu ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia, kukamilisha usimamizi wa uchumi wa dunia, na kusukuma mbele uhusiano wa kimataifa uwe wa kidemokrasia. Bw. Cheng Guoping amesema, China inaunga mkono kithabiti na kushiriki kwenye ushirikiano wa nchi za BRICS, na inatarajia mkutano wa Ufa utaweza kuanzisha uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika mambo ya kimataifa.

    Hivi sasa, Russia inavutana na nchi za magharibi juu ya masuala ya Ukraine na Syria. Akijibu swali kama mkutano huo wa BRICS utajihusisha na mvutano dhidi ya nchi za magharibi kuhusu masuala hayo, Bw. Cheng Guoping anasema:

    "Kundi la BRICS ni jukwaa la ushirikianno kati ya masoko mapya yanayoibuka na nchi zinazoendelea, linayofuatilia zaidi ni masuala ya uchumi na maendeleo. BRICS si umoja wa kijeshi au kisiasa, na wala hailengi upande wa tatu. Ushirikiano kati ya nchi za BRICS uko wazi na wa kunufaishana, ambao unaonesha moyo wa demokrasia katika mahusiano ya kimataifa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako