• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mataifa maskini yatakiwa kupunguza gharama ya kibiashara.

    (GMT+08:00) 2015-07-06 20:26:28

    Shirika la kibiashara ulimwenguni WTO imayataka mataifa maskini kujaribu kupunguza gharama ya kufanya biashara ili kujaribu kuleta ukuaji wa kiuchumi katika mataifa hayo.

    Shirika hilo limesema kuwa gharama za juu za kibiashara katika mataifa hayo zinawafukuza wawekezaji ambao wangewekeza katika mataifa hayo na kuinua uchumi wao pakubwa.

    Aidha mataifa hayo yametakiwa kufungua masoko yao na pia kuingia katika masoko ya pamoja na mataifa mengine ili kufaidika na masoko hayo.

    Baadhi ya mataifa hayo yakiwa Afrika sasa litakuwa ni jukumu la serikali za mataifa hayo kufanya mapendekezo ya kubadilisha sera za kibiashara ili kuweza kufaidika kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako