• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachagua Jin Liqun mgombea wa mkurugenzi wa AIIB

    (GMT+08:00) 2015-07-06 21:21:42

    Wizara ya fedha ya China imesema, mkutano maalumu wa mawaziri wa fedha kuhusu maandalizi ya benki ya uwekezaji wa miundombinu ya Asia AIIB uliofanyika jumamosi wiki iliyopita mjini Beijing ulipitisha utaratibu wa kuchagua wagombea wa nafasi ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo. China imemteua rasmi Bw. Jin Liqun kugombea nafasi hiyo kwa upande wa China.

    Habari nyingine zimesema, Bw. Jin ni katibu mkuu wa Sekretariet wa muda wa Benki hiyo, ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa fedha, naibu kiongozi wa kwanza wa Benki ya Maendeleo ya Asia, msimamizi wa Kampuni ya Uwekezaji wa China na mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya Fedha ya Kimataifa ya China, nafasi ambazo zimempa uzoefu wa usimamizi na uongozi katika serikali, mashirika ya kimataifa na kampuni binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako