• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyimbo ya kugombea kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi yaingia shuleni

    (GMT+08:00) 2015-11-11 11:31:42






    Wimbo wa kauli mbiu wa Michezo ya Olympiki ya Beijing ya Mwaka 2008, uitwao "Beijing Yakukaribisha" na nyimbo nyingine zinazohusu michezo hiyo ziliimbwa sana. Nyimbo hizo zilizobeba shauku ya umma kwa Michezo ya Olimpiki, zimekuwa sehemu muhimu ya urithi wa utamaduni wa Olimpiki. Kutoka maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing hadi Beijing na Zhangjiakou kushirikiana kugombea kuwa wenyeji wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2022, nyimbo zimekuwa daraja linalounganisha michezo ya Olimpiki na umma. Hivi karibuni, nyimbo za kugombea kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi kama vile "Matarajio", "Beijing", "Amsha majira ya baridi" zinapigwa sana mashuleni mjini Beijing, na kuwavutia sana wanafunzi, hata wakati huu wa majira ya joto.

    Wimbo huu "Matarajio" unaoimbwa na wanafunzi wa shule ya msingi Yangfangdian ya Beijing unaonyesha jinsi watoto wanavyopenda majira ya baridi na michezo ya majira hayo. Uimbaji wake sio mgumu, hivyo wanafunzi wanaweza kuimba baada ya kuusikia mara kadhaa.

    "Wimbo huu ni nzuri sana, naupenda sana."

    Kwa wanafunzi wengi hapa jijini Beijing, michezo ya majira ya baridi si migeni. Msichana Zhao Jialin mwenye umri wa miaka 11 ni mwanafunzi wa darasa la 5, amecheza mchezo wa kuteleza kwenye theluji kwa miaka minne. Kila wikiendi wakati wa majira ya baridi, wazazi wake wanampeleka mjini Zhangjiakou kuteleza kwenye theluji.

    "Nilianzia kuteleza kwenye theluji nilipokuwa na umri wa miaka 7 hivi, mara ya kwanza nilikuwa na wasiwasi na hofu sana, lakini baada ya kufanya sana mazoezi, siogopi tena na nafurahia sana ninapoteleza kwenye theluji."

    Tangu Beijing kuanza kugombea nafasi ya kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 2001, Shule ya Msingi Yangfangdian iliyo chini ya kamati ya elimu ya wilaya ya Haidian imezingatia kuwaelimisha wanafunzi kuhusu Michezo ya Olympiki. Naibu mkurugenzi wa kamati hiyo Bw. Zhang Yanxiang anaona moyo wa Olympiki unasaidia ukuaji wa vijana.

    "Shughuli hizi zina ushawishi mkubwa katika kuwafundisha watoto kuhusu nguvu ya umoja na kupendana, pia zinawasaidia kupata ufahamu kuhusu michezo, kuhusu dunia ilivyo na watu wa nchi mbalimbali duniani wanavyoishi. "

    Wimbo wa "Beijing" unaeleza kumbukumbu za watu wazima wa Beijing za kuteleza kwenye barafu nje ya nyumba kila inapofika msimu wa baridi wakiwa watoto. Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na viwanja vingi vya kuteleza kwenye barafu vilivyo ndani ya nyumba mjini Beijing, mchezo huo unaweza kufanyika mwaka mzima hata msimu wa joto. Mwanafunzi wa darasa la tatu Yang Qihua amepanga kufanya mazoezi ya kuteleza kwenye barafu pamoja na wanafunzi wenzake katika uwanja wa ndani ulioko karibu na shule yake.

    "Napenda sana kuteleza kwenye barafu, na mchezo huu unatuvutia sana."

    Pamoja na nyimbo kupigwa mashuleni, bingwa wa dunia wa kuteleza kwenye barafu, ambaye pia ni balozi wa kugombea nafasi hiyo Bibi Li Nina, ametembelea shule nyingi jijini Bejing kubadilishana mawazo na wanafunzi. Bibi Li amewaambia wanafunzi kuhusu maisha yake akiwa mchezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu, na ushiriki na utendaji wa wachezaji wengine kutoka China katika michezo ya Olimpili ya majira ya Baridi.

    "Picha hii ilipigwa wakati niliporuka hewani, nilipoteleza kwa FREE STYLE, yeyote aliwahi kuangalia mchezo huu? Naona wengi mnanyoosha mikono. Tuna mabingwa wengi wa dunia katika michezo ya baridi, kama vile bingwa wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2006 Bw. Han Xiaopeng, alikuwa mwanaume wa kwanza kutoka China kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, na bingwa wa Olimpiki Bibi Li Jianrou. ana bahati, siyo? Lakini alicho nacho ni zaidi ya bahati. Kama hakushinda kwenye michuano na nusu fainali, asingeweza kuingia kwenye fainali, hivyo mtu anayejiandaa vizuri ana nafasi kubwa ya kushiriki"

    Wakati michezo ya majira ya baridi ikiendelea kukua nchini China, wanafunzi wa shule za msingi wa siku hizi huenda watakuwa wachezaji au wahudumu wa kujitolea katika michezo ya Olimpili ya majira ya baridi baada ya miaka 7. Cha muhimu zaidi ni wataweza kufurahia michezo ya baridi katika maisha yao yote.

     

    "Napenda sana kuteleza kwenye barafu, inanivutia sana."

    "Kuteleza kwenye theluji kunanisisimua, naona uhuru ninapoteleza na kuruka."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako