• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuja China ni honeymooon ya pili lakini nakosa sana chakula cha nyumbani Nigeria

    (GMT+08:00) 2015-07-17 16:58:44

    Karibu sasa tusikilize hadithi ya David Ortom kutoka Nigeria ambaye anaishi hapa mjini Beijing.






    "Nilioa mwaka jana tu na nilipokuja hapa sikuwa peke yangu lakini nilikuja na mke wangu na kwa hivyo ilikuwa ni fursa nyingine ya kufurahia na pia honeymoon"

    Hii ni hadithi ya David Ortom kutoka Nigeria ambaye sasa anaendelea na kozi yake ya mwaka mmoja hapa China.

    Isipokuwa Nigeria ni yenye watu wengi Barani Afrika, kama ilivyo China na idadi kubwa ya watu duniani, bado kuna tofauti kubwa ya jinsi watu wanavyosafiri na kuishi mjini Abuja ikilinganishwa na Beijing.

    Akiwa nyumbani anatumia gari lake kusafiri kwenda kazini na shughuli mbalimbali, isipokuwa pia msongamano wa barabari ni changmoto mjini humo.

    Lakini hapa Beijing ambapo kuna zaidi ya magari milioni 5 msongamano barabarani ni jambo wanalokumbanana nalo wakaazi kila siku David anaona anaokoa muda kwa kutumia usafiri wa umma kwa sababu….

    "mabasi yanakuja kwa wakati, na taxi ziko kila mahali na bila shaka subway iko na bei yake ni nafuu. Mjini Abuja sio kila mahali taxi ama mabasi yanaweza kwenda kwa hivyo unatumia pesa nyingi kusafiri maeneo mbalimbali"

    Uwezo wa China wa kuwa na uchumi mkubwa duniani na huduma zuri za kijamii pia umekuja na changamoto zake.

    Utoaji wa gesi chafu kutoka viwandani na miradi ya kawi ya mkaa umechangia pakubwa kuchafuka kwa hewa haswa katika miji mikuu.

    Ni hali ambayo wenyeji na wageni wanakumbana nayo.

    David pia ameathirika kutokana na hali hiyo, lakini kuna jambo linalopma matumaini ya siku za baadaye.

    "Kuna kitu kimoja nimegundua kuhusu China, kwamba wanaweza kufanya kila kitu na kwa mfano unakumbuka wakati wa mkutano wa APEC mjini Beijing mwaka jana walifanya mipango ya kuhakikisha hewa ni safi angalau kwa wiki moja na hewa ilikuwa safi kweli. Kwa hivyo naamini kwamba hatua wanazochukua sasa ni zuri na zitaifanya China kuwa mahali pazuri kwa watu kuendelea kuishi na kutembelea"

    Huku usalama ukiwa umehakikishwa katika maeneo mengi ya mjini, umeme maji na intaneti masaa 24 David anaona kuna mengi yaliofanywa na serikali kuboresha maisha ya kila siku ya watu.

    Beijing machoni mwake ni kama bahari, kuna maeneo mengi ya kutembelea, mahadhari mazuri bustani na majumba yenye hifadhi za kumbukumbu majengo na maendeleo ya kiteknolojia.

    David anasema anapendezwa na jinsi wachina na hasa vijana wanavyotekeleza kazi zao na kutaka kuwa na usanifu ama ubora wa juu zaidi.

    "Kuwa hapa imenifunza mambo mengi na la muhimu ni kwamba unaweza kuanzia popote na ukafanikiwa hata kama hauko kwenye serikali-kwa sababu nafahamu wakati china ilipoanza harakati za maendeleo na hadi ilipo sasa. Nimepata pia kujua kwamba naweza kufanya lolote na nikafanikiwa kama nitajitolea. Kwa mfano mara nyingi natazama runiga za hapa China, hasa channeli za burudani na nimegundua kwamba licha ya kuwa watu wengi wanafahamu kuwa Nigeria ina talanta, hapa China pia wana vipawa hata kuliko nilivyotarajia. Wanawekeza muda na pesa kwa chochote wanachofanya na wanafanya mambo yote kwa msingi wa kitaaluma hata likiwa ndogo aje"

    Kwenye mji huu wa wakaazi milioni 20 chakula ni sehemu ya utamaduni na maisha ya kila siku hapa.

    Huwezi kufahamu hesabu ya hoteli zilizopo Beijing na pia aina ya vyakula inazidi menu yenye kurasa nyingi.

    Watu wa kusini hula tofauti na wa kaskazini na karibu kila mkoa una chakula chake-wote wakikutana beijing kutoka mikoa yote 34 mchanganyiko unakuwa mwingi.

    Licha ya kuwa David anapenda baadhi ya vyakula, lakini anaona vile vya Nigeria vinamfaa zaidi.

    "Nakosa sana aina ya mchuzi wa nyumbani uitwao Opuchu. Lakini pia mke wangu ananipikia vyakula vya Nigeria kama vile fufu kwa kutumia unga wa kichina ambao wanautumia kutengeneza baozi na ni zuri sana. Pia kuna duka moja la mama mchina ambapo tunanunua bidhaa za kupika za kiafrika kama egusi. Na jambo linguine ni kwamba napenda sana nyama ya nguruwe na niligundua kuwa wachina pia wanapenda sana nguruwe na iko hapa kwa wingi"

    Baada ya mwaka mmoja David anapanga kujifunza kichina na hatimaye kuanza kufanya biashara kwa kununua bidhaa China na kuuza Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako