• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lugha ilikuwa ni changamoto lakini Jeffrey anajitahidi kuwa stadi na kusaidia kuondoa gugu maji kwenye ziwa Victoria.

    (GMT+08:00) 2015-11-11 11:32:00






    Kila mwaka wanafunzi wengi wa Afrika wanapata msaada wa masomo kujiunga na vyuo mbali mbali nchini China.

    Lakini katika kipindi cha miezi michache ya kwanza wanakabiliwa na changamoto ya kujumuika kwenye utamaduni na desturi za watu wa China.

    Jeffrey Okundi ni mmoja wa wanafunzi kutoka Kenya ambaye amejiunga na chuo cha Sayansi cha China na kama Ronald Mutie anavyoripoti mambo kwake pia hayakuwa rahisi.

    "Tuliwaambia tunataka mafuta wakatupatia sabuni ya kuoga"

    Alipokuja China mwaka huu Jeffry Okundi kama walivyo waafrika wengi alikabiliwa na changamto ya lugha.

    Na kila walipoenda madukani mjini Beijing walipata ugumu wa kununua bidhaa na kwa jumla huu ulikuwa ni ukurasa wa maisha mapya.

    "Shida ya kwanza ilikuwa luga, nakumbuka tulipokuja, hatukuwa na vitu kama mafuta kwa sababu hataka kubeba vitu na tunaweza kununua huko China, kwa hivyo tulipoenda kwa duka tukawaambia tunataka mafuta wakatupatia sabuni ya kuoga kwa sababu hawakuelewa. Ilitubidi tutumie ishara ya mikono. Na shida ingine ilikuwa ni kuzoea utamaduni mpya, kwa mafano kenya jinsi watu wanavyovaa ni tofauti na hapa amnapo tuliona wanavaa nguo fupi na hakuna mtu anashughulika"

    Lakini pia alipata mambo mengine ya Beijing yanayofana na yale ya Nairobi kama vile kwenda kwenye bustani kutembea.

    Jeffrey hata hivyo sasa anaweza kuwasilinana vyema kwa lugha ya kichina na ameanza kufaniskisha ndoto yake katika masomo.

    Anasomea sayansi ya kukabiliana na mimea ama wanyama vamizi kwenye mvumo wa ikolojia.

    Mifano ya mimea na ama wanyama vamizi ni kama vile gugu maji katika ziwa Victoria ambayo inatatiza shughuli za uvuvi na uchukuzi kwenye ziwa hilo kubwa zaidi barani Afrika.

    "Kuhusu gugu maji tumejaribu njia nyingi za kuiangamoiza lakini zimekata ndio nilionelea nikikuja huku naweza kutumia njia mpya. Na moja wa njia hizo ni kutumia alama za kimaumbile ambayo itatusaidia kujua ni kwa nini mimea hio inaenea na tukijua basi tunaweza kutumia njia za kisayansi kuiondoa"

     

    Na sio tu gugu maji ambayo analenga kuangamiza Jeefrey.

    Kaskazini mwa kenya pia kuna mmea mwingine vamizi.

    "kuna mea wa mathenge na kwa upande wa wanyama kuna samaki aina ya nile perch katika ziwa Victoria ambaye anapunguza wingi wa Tilapia. Mmea huo wa mathenge sasa umechukua mahali pa miti ambayo ilikuwa inamea kwenye sehemu ile na pia kumekuwa na kesi wakati mmoja kwamba mbuzi wanapokula mmea huo wanapoteza meno. Kwa hivyo inakuwa shida kwa wafugaji kama jamii ya wamasaai na wakalenjin"

    Jeffrey ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 70 ambao wamepata msaada wa masomo mwkaa huu kujiunga na vyuo mbali mbali nchini China.

    Ni msaada ambao unawawezesha wanafunzi wengi haswa kutoka jamii za mapato ya chini kuendelea na masomo yao lengo kuu lilikuwa ni kuchangia sekta mbalimbali wanapokamilisha masomo yao.

    Na kutokana na mfumo tofatuti wa kufundisha vifaa bora katika katika chuo chake, Jeffrey anatarajia kupata ustadi bora kwa ajili ya kazi yake.

    "Hapa sio kusoma kwa darasa tu mbali kuna masomo mengi ya nyanjani. Na pia kuna waalimu ambao ni spesheli kwa masomo fulani hivyo tukifikia na inatufanya tuelewe zaidi. Ukilinganisha na chuo nilichosomea Nairobi utaona kwamba tuko na waalimu wazuri lakini raslimali ni kidogo na kila darasa kuna wanafunzi kama 300 lakini hapa ni kama 12 kwa darasa moja"

    Serikali ya china imekuwa ikitoa misaada ya masomo kwa wanafunzi wa kenya kila mwaka tangu mwaka wa 1982.

    Kwa sasa kuna wanafunzi 200 wa kenya wanaosomea vyuo mbalimbali nchini china wakifadhiliwa na serikali ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako