• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafanyibiashara wa  China wanashauri vizrui kuhusu bidhaa kabla ya kuuza.

    (GMT+08:00) 2015-11-11 11:32:00






    Kuishi kwingi ni kuona mengi na unapoembea unaongeza maarifa maishani.

    Na pia unafahamu mambo yanayoweza kuisaidia jamii na nchi yako kwa jumla.

    Ndio hadithi ya Caroline kutoka Kenya kama anavyoripoti Ronald Mutie

    Hadithi ya Carol Wanini Kutoka Kenya ina kurasa nyingi.

    Licha ya kwamba umri wake ni mdogo, amefanikiwa kufanya mambo mengi na kuzoea mazingira, tamaduni, watu na nchi tofauti haswa mashariki ya kati na hapa China.

    "Mwanzoni nilikuwa nafanya biashara na kufunza katika shule mbalimbali, kutuma vitu kutoka China lakini baadaye nikaamua kusoma hapa China. Sasa niko katika chuo cha Liaoning nasomea Uchumi na Biashara ya kimataifa"

    Miji aliofanya biashara na kufunza ni pamoja na Yiwu na Guangzhou.

    Kabla ya kuanza kuwafunza watoto kiingereza yeye mwenyewe alijifunza kichina ili kuweza kuwasiliana nao kwa urahisi.

    Anawapenda watoto na hivyo aliichukulia kazi hiyo kama uraibu.

    "sio vigumu kwa sababu hao watoto wanataka kujua na ukiwa mwalimu kama mtu anataka kujua unafurahia kumwelezea. Pia unawaweka karibu ili kujua utamaduni wao. Pia hapa sio kama vile tunafunzwa kule nyumbani ambapo wanafunzi wanamuogopa sana mwalimu, siku zote walipenda kukaa karibu na mimi na hakukuwa na tatizo"

    Lakini licha ya kuwa kulikuwa na fursa nyingi za biashara, na kazi za ualimu, Carol aliamua kujiunga na masomo.

    Anasema wakati mwingine unaweza kupata pesa kila siku lakini bila akiba ya kitu muhimu kama masomo huwezi kuhakikisha siku za usoni.

    Alifanya utafiti wa mahali atakapoendelea na masomo yake ya chuo kikuu kwa sababu zinazoendana na mahitaji yake.

    "China ndio iko na uchumi ulio juu kwa sasa na wakati nilikuwa nafanya biashara nilitaka kuelewa zaidi kuhusu mambo yote ya biashara hapa China "

    Akiwa mjini Yiwu na Guanzhou alipokea maombi ya wateja kutoka Kenya wakimweleza bidhaa wanazotaka.

    Kazi yake ilikuwa ni kuzitafuta, kuwafahamisha bei na kufanya mpango wa kuzituma hadi nyumbani.

    Lakini pia alikuwa na wakati mgumu haswa maswali mengi kutoka kwa watu walio na dhana kuwa bidhaa nyingi za China ni gushi jambo ambalo sasa analieleza dhahiri.

    "Wachina vile wanavyofanya ile biashara yao inakuvutia zaidi , akitaka kukuuzia bidhaa anakuambia manufaa yake na kwa nini uinunue. Watu wanasema bidhaa za china nigushi lakini ukienda pale atakueleza kuna toleo la kwanza na la pili. Toleo la pili ndio gushi na hivyo anakushauri ununue toleo la kwanza. Kwa hivyo niliweza kujua hayo matamshi ya kibiashara na niliyapenda sana"

    Kwa wingi waafrika wananunua bidhaa kama za ujenzi, nguo, elektroniki na mashine.

    Hata hivyo, Caroline alipata oda nyingi za bidhaa za wanawake kama vile mifuko, mapambo, na viatu

    Ugumu wa kufanya biashara kati ya china kama anavyosema Carol ni lugha na muda zinaochukua bidhaa kufika nyumbani.

    Inachukua kama siku 40 kusafirisha shehena kwa njia ya meli ama wiki moja kwa ndege lakini bei yake ni ghali mno.

    Akiwa sasa anafahamu lugha ya kichina na kupata masomo hapa mjini Beijing Caroline ameweka matumaini makubwa ya kujinufaisha na fursa za kibiashara zinazoendelea kuongezeka kati ya pande zote mbili.

    "Masomo yangu yatanisaidia kuchangia kukua kwa uchumi wa Kenya kwa kufanya biashara kati ya Kenya nan chi nyingine sio china tu. Nataka kuelewa kinachohitajika katika kila soko "

    Mbali na china caroline amewahi kufanya kazi nchini Saudi Arabia, kutembelea Qatar na kila mahali amepata uzoefu tofauti.

    Anaamini kwamba licha ya kuwa China na Afrika zina uchumi unaoendelea, bado Afrika inaweza kujinufaisha na teknolojia na ujuzi wa kuendeleza sekta ya viwanda na miundo mbinu kutoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako