• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa rangi ya kijani, Altai

    (GMT+08:00) 2015-07-22 11:37:30

    Eneo la Altai la mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, magharibi mwa China limechukuliwa kuwa ni chimbuko la michezo ya kuteleza kwenye barafu. Altai inapakana na eneo lenye vivutio vya maumbile la Kanas, ina mandhari nzuri na kiwango cha upandaji wa miti ni cha juu. Serikali na wananchi wa huko wanatilia maanani sana uhifadhi wa mazingira, na kufanya juhudi kuzuia anga ya bluu na maji safi visichafuliwe.

    Mji wa Altai uko kusini mwa Mlima wa Altai, na mto Kelan unapita mjini humo, bustani zimeenea hapa na pale. Bustani ya misitu inayopewa jina la mzalendo wa kabila la Kazak Shalifuhan Genenshan Kukudaiyev inatembelewa na watalii wengi kila siku, na inasifiwa kuwa ni chanzo cha upandaji wa miti katika mji huo. Afisa wa serikali ya mji huo Yang Kaijing anasema,

    "Yeye alikuwa ni mtu mwenye mapenzi mema na taifa letu. Baada ya kujifunza utamaduni wa kisasa wa Russia, alikuja China, akafungua shule kadhaa, na kupanda miti katika mji wa Altai. Miti iliyopo katika bustani hiyo ilipandwa kwa mpango wake, na kujengwa kuwa eneo linalotoa hewa nyingi ya oxygen. Awali bustani hiyo iliitwa Hua Lin, lakini sasa tunaiita kwa jina lake, yaani bustani ya Shalifuhan."

    Kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi wa Altai, idadi ya watu wa mji huo pia inaongezeka. Ili kuboresha maisha ya wakazi na kuongeza fursa za maendeleo, serikali ya mji huo imetekeleza miradi ya ujenzi katika sehemu ya kusini mwa mji huo. Mkurugenzi wa idara ya ujenzi wa mpango wa miji na vijiji ya Altai Gao Jianhua anasema, mpango wa eneo jipya umekamilishwa kwa pamoja na mashirika husika ya Uingereza na ya China, na kuonesha vya kutosha fikra ya uhifadhi wa mazingira na sifa ya "mji unaofaa kuishi".

    "Tulipoanza kutekeleza mpango huu, tulitumia mwaka mmoja kupanda miti kwenye eneo la hekta 200 katika mlima uliopo karibu. Miti imepandwa katika asilimia 42 ya ardhi za eneo zima la kusini lililopangwa, na katika miaka miwili na mitatu ijayo, tutaendelea kupanda miti ili kupamba vizuri zaidi eneo hilo."

    Mbali na kupanda miti mjini, tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita, mji wa Altai ulianzisha mradi wa upandaji miti katika milima isiyo na miti ukiwemo mlima wa Jiangjun, na sasa ufanisi umeonekana kwa hatua ya mwanzo. Xu Xiuqi mwenye umri wa miaka 63 ni mshiriki na shuhuda wa mchakato huo. Anasema,

    "Awali huu ni mlima ulikuwa na miamba, na ilikuwa vigumu sana kuchimba shimo. Baada ya kulipua mwamba huo kwa mabomu, tulifanya usafi, halafu tukaweka udongo na kupanda miti. Baada ya miaka mitano, miti iliyo katika mlima wa Jiangjun imefikia laki 7. Sasa mlima huo umekuwa na rangi ya kijani, na katika siku za baadaye tutaendelea kufanya milima kama huo iliyo karibu na mji wa Altai kuwa ya rangi ya kijani. Watu tunaowafahamu ama tusiowafahamu wote wanasema mlima huo ni mzuri, umekuwa rangi ya kijani na miti inakua vizuri. Wakati huo najisikia vizuri, na kuridhika."

    Mbali na kupanda miti kwenye milima hiyo, mji wa Altai umesafisha maji taka yanayotoka kwa wakazi elfu 80 ili kumwagilia milima isiyo na miti yenye eneo la hekta 533, ili kuepusha maji hayo kuingia katika mto Kelan na kuchafua maji ya wakulima na wafugaji wanaoishi sehemu za chini. Naibu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa usafi wa maji taka ya Altai Azat Abula amesema mradi huo umeonesha mwamko wa serikali wa kulinda mazingira, na pia utanufaisha mazingira na jamii.

    "Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2012, na sasa manufaa kwa mazingira na jamii yameanza kuonekana. Bwawa la kusafisha maji taka limekuwa kivutio muhimu cha utalii, zamani hapa hakukuwa na kitu chochote, lakini baada ya kuvuta maji hapa, limekuwa eneo muhimu wanalokaa wanyama na ndege wa aina mbalimbali."

    *********************************

    Mji wenye neema wa Changji

    Wilaya inayojiendesha ya Changji iko sehemu ya chini ya Ziwa Tianchi, ambalo ni kivutio maarufu cha utalii mkoani Xinjiang. Wakati mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Uyghur unakaribia kutimiza miaka 60 tangu uanzishwe, shughuli mbalimbali za jimbo hilo zimeendelezwa vizuri.

    Ukiendesha gari kutoka mji mkuu wa Xinjiang, Urumqi, inachukua muda wa saa 1 tu kuwasili mji mkuu wa jimbo la Changji. Hivi sasa maendeleo ya kasi ya miji hiyo miwili inawafanya watu washindwe kutambua tofauti zao, na mji huo Changji pia umesifiwa kuwa Ua la Urumqi. Unaweza kufahamu kwa kina maendeleo ya Changji ukitembelea eneo la taifa la sayansi ya kilimo lenye hekta 420 mjini humo, ambako teknolojia mbalimbali za hali ya juu za kilimo cha kisasa zinatumika. Mkurugenzi wa kamati ya usimamizi ya eneo hilo Bao Zhenxing amesema wanataka kujenga eneo hilo kuwa bonde maarufu la kilimo cha kisasa duniani.

    "Tuna nyumba kitalu nyingi, na mimea inayooteshwa katika nyumba hizo imeingizwa kutoka sehemu mbalimbali nchini China, na baadhi yao inatoka nje ya nchi. Pia tunakuza uchumi kwa kuandaa maonyesho, na kila mwezi kuna maonyesho yanayofanyika hapa. Kwa hivyo, kitu cha kwanza wanachoona watu wanaokuja Xinjiang ni maonesho ya "Xinjiang Nzuri" ili waweze kuhisi mvuto wa mkoa huo."

    Maendeleo ya kilimo cha kisasa hayawezi kutengana na maandalizi ya wataalam wa kilimo. Chuo cha kilimo cha Xinjiang, ambacho awali kilikuwa shule ya kilimo ya Changji kimeftoa mchango mkubwa katika sekta hiyo. Wahitimu wa chuo hicho wanaweza kuzoea kwa urahisi mahitaji ya kazi za uzalishaji wa kilimo cha kisasa, na wanaweza kujiajiri au kuwa nguzo muhimu katika kampuni za kilimo. Mkuu wa chuo kicho Wang Yi anasema chuo kicho sio tu kinaandaa wataalamu wa kilimo kwa Xinjiang, pia kitatumia fursa za mkakati wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kuhamisha teknolojia na mimea yao kwa nchi za Asia na Kati.

    "Tuko mbioni kuchagua mahali pa kujenga kituo cha kielelezo na mafunzo ya kilimo cha kisasa katika nchi za Asia na Kati. Kwanzo ni kuweka mfano, pili kutoa mafunzo kwa watu. Lengo letu la kuanzisha kituo hicho ni kuitikia mkakati wa 'Ukanda Mmoja na Njia Moja", kupeleka ufundi kwa nje, kwani ufundi ni ghali zaidi kuliko bidhaa. Pia tunauza mibegu ya mimea tuliyoboresha. Chuo cha kilimo ndicho kinaotesha aina mpya za mimea na ufundi."

    Msemaji wa idara ya habari ya serikali ya jimbo la Changji Miu Xia amesema ana matumaini kuwa katika siku za baadaye, Changji itatumia nguvu zake kujijenga kuwa mji wenye ustawi na neema, umaalamu wa kikabila, pamoja na mazingira bora ya kuishi, na kuendeleza sekta mbalimbali za jimbo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako