Matakwa:
1. Maingizo yanatakiwa kulingana na kaulimbiu na kuonesha maudhui mazuri na maadili yanayofaa
2. Idadi ya nakala zinazowasilishwa haina ukomo, lakini aina kuu ni maandishi. Matakwa kwa idadi ya maneno ni 70-100 au 140-180 (maneno yanahesabiwa kwa ajili ya matangazo ya sekunde 30 au dakika moja)
3. Kazi zinazowasilishwa ziwe za Kiingereza.
4. Hairuhusiwi kuhusisha habari zisizohusiana na wazo kuu la usanifu, kama vile taarifa binafsi ya washiriki. Na kazi inayotumwa haitakiwi kutumwa kwenye shindano lingine.
5. Washiriki wanatakiwa kutoa taarifa halisi na sahihi na njia ya mawasiliano kama inavyotakiwa kwenye fomu ya maombi. Kama taarifa hizo si sahihi na kamili, kamati ya maandalizi ina haki ya kumwondoa mshiriki.
Njia za kutuma:
Pakua fomu ya maombi kutoka kwenye safu ya shindano hili katika tovuti ya Kiswahili ya CRI Online (https://swahili.cri.cn/ ).
Halafu tuma kazi kama kimbatanisho kwa barua pepe Kiswahili@cri.com.cn na psa@cri.com.cn. Njia nyingine za kutuma hazitakubaliwa.
|