• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la 18 la Filamu la Zanzibar

    (GMT+08:00) 2015-07-24 14:54:57

    Msikilizaji mpendwa, karibu katika kipindi cha Utamaduni Wetu. Tamasha la 18 la filamu la kimataifa ya Zanzibar ZIFF limeanza hivi karibuni katika uwanja wa Mji Mkongwe Zanzibar. Wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania na pamoja na watalii wanajumuika kwa ajili ya tamasha hilo. Tamasha hilo lenye kauli mbiu "Mawimbi na Matumaini" litafanyika kwa siku tisa, ambapo filamu 99 zilizotengenezwa na waandaaji 65 kutoka nchi 35 zinatarajiwa kuoneshwa. Hatimaye, makundi matano ya waamuzi watatoa tuzo 22 kwa filamu bora.


    Mratibu wa tamasha hilo, Martin Mhando anasema, ataitumia fursa hiyo kuhimiza maendeleo ya tamasha hilo. Bw. Mhando anasema,

    "Tamasha ya filamu ya kimataifa ya Zanzibar ni shughuli muhimu katika historia ya Zanzibar, ambayo haiwezi kusahauliwa. Kaulimbiu ya mwaka huu ni 'Mawimbi na Matumaini'. Kama tunavyojua, tunaishi kisiwani Zanzibar, tunakabiliana na mawimbi yanayotoka kwa pande mbalimbali. Natumai kuhimiza maendeleo ya tamasha ya filamu na nchi yetu kupitia mawimbi ya tamasha ya ZIFF. Leo sote tunavaa mavazi nyeupe, amabyo yanamaanisha nchi yetu ni nchi yenye amani na utulivu zaidi barani Afrika na kote duniani. Karibuni ZIFF, karibuni Zanzibar, asanteni."

    Mwaka huu siku ya ufunguzi wa tamasha la ZIFF iligongana na sikukuu ya IDD, kwenye hotuba yake, mwenyekiti wa tamasha la ZIFF Mahmoud Kombo amesema, kukutana kwa shughuli hizo mbili kunawavutia watalii wengi zaidi, ambako kuna maana kubwa kwa ustawi wa utamaduni na uchumi wa Tanzania.

    "Leo ni Julai 18, na ZIFF imetimiza miaka ya kumi na nane. Na leo pia tunasherehekea sikukuu ya Idd hapa Zanzibar. Tamasha ya ZIFF kila mwaka inawavutia watalii zaidi ya elfu nne kutoka nchi mbalimbali duniani, leo pia ni sikukuu ya Idd hapa Zanzibar, nina imani kuwa mwaka huu watalii wengi zaidi watakuja hapa. Hivyo ZIFF inaweza kustawisha utamaduni na uchumi wa nchi yetu, na kuwafanya marafiki wengi zaidi kufahamu nchi na utamaduni wetu. ZIFF imepita miaka 18, ambayo inawafanya marafiki wengi kuifahamu Zanzibar yenye mandhari safi na kuipenda. Nafikiri nyote mtaona uzuri wa Zanzibar"

    Baadhi ya nchi zilizowasilisha filamu kwenye mashindano ni Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Marekani, Ujerumani na Ufaransa. Mratibu wa tamasha hilo Bw. Mhando anasema filamu zinazohusiana na kupambana na ubaguzi wa rangi zinapewa kipaumbele katika tamasha hilo. Filamu ya Selma kutoka Marekani, Sarafina kutoka Afrika Kusini, Samaki Mchangani kutoka Tanzania na Septemba kutoka Kenya zote zinahusu mada hiyo.

    Kati ya filamu zinazoshiriki kwenye tamasha hilo, 16 zimetengenezwa nchini Tanzania. Bw. Mhando anafurahia kuona tamasha hilo linastawisha soko la filamu la Tanzania, kuhimiza maendeleo ya utengenezaji wa filamu Tanzania, na kutoa fursa nyingi zaidi kwa watanzania kutazama filamu kutoka nchi mbalimbali duniani.

    Katika ufunguzi, watalii wengi kutoka nchi mbalimbali duniani wanakuja hapa, Bibi Rose kutoka Uholanzi ni mmojawapo.

    "Naitwa Rose, natoka Uholanzi. Leo tamasha hili linafunguliwa. Tamasha hili linavutia sana, kwa sababu linahusu utamaduni na filamu, hapa kuna filamu, muziki na sanaa kutoka sehemu mablimbali duniani. Naona kuna umuhimu mkubwa wa kufanya tamasha la filamu ambalo linawashirikisha watu wengi kutoka nchi mbalimbali, na wengi wao wamekuja kwa ajili ya tamasha hilo. Tamasha la filamu linaunganisha marafiki kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani. Nilikuwa nadhani Afrika ni sehemu maskini, lakini leo mawazo yangu yamebadilika. Naona tamasha la filamu litawapatia watu wengi ufahamu mpya kuhusu Tanzania."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako