• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa China akutana na katibu mkuu wa Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake

    (GMT+08:00) 2015-07-28 17:37:41

    Makamu wa rais wa China Li Yuanchao amekutana na katibu mkuu wa wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake Gertrude Mongella leo hapa Beijing.

    Li amesema Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika mjini Beijing mwaka 1995 una umuhimu mkubwa na athari kubwa. Anatarajia kuwa mkutano wa kilele wa wanawake duniani utakaoandaliwa kwa pamoja na China na Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu katika makao makuu ya Umoja huo huko New York utapata mafanikio, na kuendelea kuhimiza utekelezaji wa "Azimio la Beijing" na "Mwongozo wa Utekelezaji". Pia anatumai kuwa mkutano huo utasukuma mbele maendeleo ya wanawake na kutimizwa kwa malengo ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

    Mongella amesema anatarajia kuwa China itachukua nafasi muhimu zaidi katika kuwawezesha wanawake na kuimarisha zaidi mawasiliano kati ya Tanzania na China, na Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako