• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Kenya watoa mwito wa kutumiwa kwa mbinu mpya ili kulidhoofisha kundi la Al Shabaab

    (GMT+08:00) 2015-07-30 16:38:36

    Wataalamu wa masuala ya usalama, wameitaka jumuiya ya kimataifa kutumia mbinu mpya zenye uvumbuzi katika kupunguza nguvu za kundi la kigaidi la Al Shaabab nchini Somalia. Katika miaka minne iliyopita kundi hilo mshirika wa AL QAIDA, limekuwa likipambana na vikovyo cya tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM na vikosi vya jeshi la Somalia katika udhibiti wa sehemu kubwa ya eneo la nchi hiyo

    Kundi hilo limeonesha uwezo mkubwa wa kubadilika na kufanya mashambulizi ndani ya Somalia na kwenye nchi jirani, licha ya jeshi la AMISOM kudhoofisha miundo mbinu yake. Katika mwezi wa Ramadhani kwa mfano, kundi hilo liliimarisha mashambulizi yake dhidi raia na vikosi wa AMISOM. Ili kujibu mashambulizi yake AMISOM kwa kusaidiwa na ndege za Marekani walishambulia eneo linalodhibitiwa na kundi hilo kusini mwa Somalia kwa muda wa wiki mbili, katika operesheni iliyosababisha vifo vya wapiganaji 72 wa kundi hilo, wakiwemo viongozi muhimu wa kundi hilo.

    Licha ya kupoteza makamanda wake, Al Shaabab imerejea upya na kufanya shambulizi la bomu la kujitoa mhanga siku ya jumapili katika hotel yenye ulinzi mkali ya Jazeera Palace mjini Mogadishu. Watu 15 akiwemo mfanyakazi wa ubalozi wa CHINA wamethibitika kuuawa kwenye shambulizi hilo.

    Wachambuzi wa masuala ya usalama, wanaona serikali ya Somalia na Jumuiya ya kimataifa zinatakiwa kuwa tayari kwa mapambano ya muda mrefu dhidi ya wapiganaji wa Al Shaabab.

    Mtaalamu wa masuala ya amani na usalama wa KENYA Bw Fred Nyambera, anasema juhudi za kutokomeza kundi la AL SHAABAB kwa sasa zimepata mafanikio madogo hivyo kunahitajika mabadiliko ya muundo.

    Mtaalamu huyo analaumu siasa za kikanda na kugombea rasilimali kuwa chanzo cha migogoro katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Pia amezilaumu nchi za magharibi kwa kutilia mkazo matumizi ya nguvu katika kutokomeza kikundi cha Al Shaabab na washirika wake.

    Anasema "Mataifa ya magharibi kwa namna nyingine yanachangia kushindwa kwa serikali ya Somalia kwa sababu ya kuweka suluhisho la kivita lisilo na ufanisi. Matokeo yake makundi kama Al Shaabab yamejitokeza kupinga kile kinachoonekana ni utawala wa kimagharibi kimawazo, kiitikadi, kiuchumi na kiutamadauni."

    Mwanazuoni wa dini ya kiislamu nchini Kenya Profesa Hassan Nandwa amesisitiza kuwa suluhisho la kisiasa linahitajika haraka dhidi ya tishio la Al Shaabab. Anaona ni lazima kuwe na jitihada za kuandaa makubaliano nao pamoja na mazungumzo ya kitaifa kwa kutumia majukwaa ya kikabila na viongozi wa kidini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako