• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabaki ya ndege yaliyopatikana kisiwa cha Reunion yanawezekana kuwa ya ndege ya Mayasyia

    (GMT+08:00) 2015-07-31 11:00:00

    Waziri mkuu wa Malaysia Bw Najib Razak amesema mabaki ya ndege yaliyopatikana kwenye ufukwe wa kisiwa cha Reunion yanawezekana kuwa ni ya ndege aina ya Boeing 777, lakini uchgunzi zaidi unatakiwa kufanyika ili kujua kama ni ya ndege ya MH370 ya Malaysia iliyopotea.

    Mabaki ya ndege yaliyopatikana kwenye kisiwa cha Reunion yatasafirishwa kwenda Ufaransa kwa uchunguzi zaidi, mabaki hayo yanatarajiwa kuwasili mjini Toulouse Ufaransa kesho. Shirika la uchunguzi wa ajali za ndege la Ufaransa lilikuwa linachunguza mabaki hayo kwa kushirikiana na wataalamu wa Australia na Malaysia. Vyombo vya habari vya huko vimesema mabaki yaliyopatikana ni sehemu ya ndege na begi moja ambalo bado limefungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako