• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Kenya Airways lapata hasara ya dola za kimarekani milioni 252 katika mwaka wa bajeti uliopita

    (GMT+08:00) 2015-07-31 11:08:05

    Shirika la ndege la Kenya Airways limtangaza kuwa katika mwaka wa bajeti uliopita ambao ulisha Machi 31 mwaka huu, shirika hilo lilipata hasara ya dola za kimarekani milioni 252 ambayo ni mara 6 zaidi ya kiwango cha hasara cha mwaka mmoja uliotangulia.

    Meneja mtendaji wa shirika hilo Mbuvi Ngunze amesema hasara hiyo kwa kiasi kikubwa inatokana na ushindani mkali na mashirika ya ndege ya nchi za mashariki ya kati na gharama kubwa za uendeshaji wa shirika lake.

    Ngunze pia amesema sababu nyingine ni kwamba, idadi ya watalii imepungua kutokana na baadhi ya nchi za magharibi kutoa tahadhari ya kutalii nchini Kenya baada ya mashambulizi ya kundi la al-Shabaab kutokea nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako