• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la 18 la Filamu la Zanzibar lafungwa

    (GMT+08:00) 2015-07-31 13:55:02

    Tamasha la 18 la filamu la kimataifa la Zanzibar ZIFF limefanyika hivi karibuni huko Zanzibar, Tanzania. ZIFF ni tamasha kubwa zaidi la filamu, muziki na sanaa katika Afrika Mashariki, na linashirikisha wasanii wapya kutoka nchi mbalimbali duniani.


    Kila mwaka, baadhi ya filamu nzuri zaidi kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani zinaoneshwa kisiwani Zanzibar. Kutoka filamu za kimataifa na filamu fupi za kienyeji zote zinaoneshwa, tamasha hilo lina historia ndefu ya kuonesha filamu zenye sifa nzuri kutoka nchi mbalimbali duniani. Filamu zinafuata kaulimbiu ya mwaka, ambayo kwa mwaka huu ni "Mawimbi na njozi ya matumaini", na kuingia katika mashindano ya tuzo za aina tofauti. Usiku wa siku ya mwisho ya tamasha hilo ni usiku wa kutoa tuzo.

    Katika tamasha la mwaka huu, filamu 99 zilizotengenezwa na waandaaji 65 kutoka nchi 35 zilioneshwa, na makundi tano ya waamuzi yalitoa tuzo 22 kwa filamu. Baadhi ya nchi zilizowasilisha filamu kwenye mashindano ni Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Marekani, Ujerumani na Ufaransa. Mratibu wa tamasha hilo Bw. Mhando anasema, filamu zinazohusiana na kupambana na ubaguzi wa rangi zinapewa kipaumbele katika tamasha hilo. Filamu ya Selma kutoka Marekani, Sarafina kutoka Afrika Kusini, Samaki Mchangani kutoka Tanzania na Septemba kutoka Kenya zote zinahusu mada hiyo. Kati ya filamu zilizoonyeshwa kwenye tamasha hilo, 16 zimetengenezwa nchini Tanzania.

    Kwa upande wa muziki, ZIFF iliandaa sherehe nzuri zaidi kisiwani Zanzibar. Maonesho mbalimbali ya muziki, ngoma na DJ yanafanywa kwa wiki mbili kisiwani humo, na kukusanya wasanii kutoka bara zima la Afrika.

    Haya, msikilizaji sasa tunakuletea matokeo ya baadhi ya tuzo muhimu za Tamasha la ZIFF la mwaka huu. Filamu iliyopata tuzo ya Bi Kidude yaani tuzo ya mwenyekiti ni filamu kutoka Ethiopia inayoitwa "Price of Love", mwandaaji wake ni Hermon Hailay. Flimu iitwayo "Every Day Is A Small Day" kutoka Ufaransa ilipewa tuzo maalumu ya kundi la waamuzi, na mwandaaji wake ni Albane Fioretti.

    Tuzo ya filamu nzuri zaidi inayoonesha hali halisi ilikabidhiwa kwa filamu kutoka Marekani "Papa Machete" iliyoandaliwa na Jonathan David Kane. Mwandaaji kutoka Tanzania Ekwa Msangi amepata tuzo ya katuni nzuri zaidi kutokana na katuni yake iitwayo "Soko Sonko". Mwandaji kutoka Kenya Gilbert Lukalia amepata tuzo ya msanii hodari wa filamu wa Afrika Mashariki kutokana filamu yake "Strength of a woman". Tuzo ya Jahazi ya fedha ilikabidhiwa kwa filamu ya "Simshar " iliyotengenezwa na mwandaaji kutoka Malta, Rebecca Cremona. Filamu inayopata tuzo ya jahazi ya dhahabu ni filamu ya "Wazi?FM" ambayo iliandaliwa na Faras Cavallo.

    Mbali na tuzo hizo muhimu, tuzo ya mafanikio ya maisha ilikabidhiwa na wasanii wawili Bi. Fatma Alloo na Hassan Mitawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako