• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kifo cha kiongozi wa kundi la Taliban Mullah Mohammad huenda kikaleta mgogoro wa kugombea uongozi ndani ya kundi hilo.

    (GMT+08:00) 2015-07-31 16:26:18

    Jumatano wiki hii serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban walitangaza kuwa kiongozi wa kundia Taliban Mullah Mohammad Omar alifariki mwaka 2013 kwenye hospitali moja nchini Pakistan, lakini habari kuhusu kifo chake zilifanywa siri ili kuepusha mgogoro ndani ya kundi la Taliban. Wachambuzi wa Afghanstan wanasema kutangazwa kwa habari kuhusu kifo cha Mullah Mohammad kunaweza kuleta mgawanyo kwenye safu ya uongozi wa kundi la Taliban na kuleta mpasuko kwa kundi hilo.

    Ikulu ya Afghanistan imetoa taarifa rasmi ikisema serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan ina taarifa za kuaminika, na imethibitisha kuwa kiongozi wa kundi la Taliban Mullah Mohammad Omar alikufa April 2013 nchini Pakistan. Mchambuzi wa masuala ya siasa Jawid Kohistani anasema mauti ya Mullah yataleta mgogoro wa uongozi kwa kundi la Taliban. Bw Kohistani anasema Mullah Omar alipata uhalali kutoka katika baraza la wanazuoni wa dini katika majira ya joto mwaka 1996, ambapo wafuasi wake walimpatia jina la Amir al- Muminin lenye maana kamanda wa imani.

    Bw Kohistani anasema baada ya kifo chake, mrithi atahitaji kupewa uongozi toka kwa baraza, ingawa kwa muda huu ni vigumu kwa Taliban kufanya baraza la kumchagua kiongozi mpya.

    Mullah Omar hakuonekana hadharani tangu majeshi ya Marekani yafanye uvamizi na kuangusha utawala wake mwaka 2011. Serikali ya Marekani ilitangaza zawadi ya dola milioni 10 za Marekani kwa taarifa itakayosaidia kukamatwa kwake.

    Mullah Omar alianzisha mapambano ya kundi la Taliban Kusini kwenye jimbo la Kandahar nchini Afghanistan mwaka 1994 na kutangaza himaya yake ya kiislamu baada ya kuuteka mji wa Kabul mwaka 1996. Amekuwa akiongoza uasi wa kumwaga damu baada ya kuanguka kwa serikali ya Taliban mwaka 2001, ambapo alianzisha upya itikadi ya waislamu wenye msimamo mkali katika nchi hiyo iliyoathiriwa na vita katikati mwa bara la Asia.

    Bw Zulmai Khalilzad mjumbe wa zamani wa Marekani nchini Afghanistan anasema hakuna mtu sahihi miongoni mwa viongozi wa Taliban anayeweza kuchukua nafasi ya Mullah Mohammad Omar na uzito wake kisiasa, kwani wanachama wengi wa Taliban walitii amri za Mullah Omar kwa miaka mingi iliyopita.

    Wakati Bw Khalilzad akibainisha kuwepo ugumu kupata kiongozi wa kundi hilo, mchambuzi mwingine Bw Babrak anasema mtoto mkubwa wa kiume wa Mullah Omar na naibu kiongozi wa Taliban Mullah Akhtar Mohammad Mansoor ni miongozi mwa watu wanaoweza kumrithi Mullah Omar.

    Pia ameitaka serikali ya Afghanistan kutumia fursa hiyo kuongeza juhudi katika makubaliano ya mazungumzo ya amani na kundi la Taliban. Maoni hayo yamekuja wakati kuna taarifa za kuahirishwa kwa awamu ya pili ya mazungumzo ya amani kati ya wawakilishi wa Taliban na serikali ya Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako