• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake wilayani Tarime nchini Tanzania wahamsishwa kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe mikopo

    (GMT+08:00) 2015-07-31 19:05:28

    Umoja wa wanawake wilayani Tarime Mkoani Mara nchini Tanzania umetakiwa kujiunga katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia mikopo na kujikwamua kimaisha kwa kuanzisha biashara.

    Katibu Uchumi wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara John Gimunta alisema hayo kwenye semina ya UWT ya wajasiriamali ambayo iliandaliwa na mwenyekiti wa umoja huo Paulina Monanka kwa ajili ya kuwaelimisha wanawake ili kujikomboa kutoka katika wimbi la umaskini. Gimunta ameongeza kuwa Serikali ina uwezo tu wa kutoa fedha kwa vikundi ambavyo vinatambulika kisheria. Gimunta pia amewataka wanawake kujifunza kuwa na tabia ya kurejesha mikopo pindi wanapokopeshwa ili kuwa rahisi na wengine kupata mikopo.

    Semina hiyo inaenda sambamba na kuelimisha wanawake wa umoja huo juu ya ujenzi wa jumuia ya wanawake kuwa chombo muhimu kwa maadili ya uongozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako