• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yasaini mkataba wa kukusanya pato la shilingi trilioni 12.4 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2015-07-31 19:06:16

    Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), imesaini mkataba wa makubaliano ya kukusanya mapato ya Sh trilioni 12.4 za kitanzania katika mwaka huu wa fedha. Mkataba huo ulisainiwa Dar es Salaam jana kati ya mamlaka hiyo na Wizara ya Fedha, ambapo, upande wa TRA uliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka hiyo, Bernard Mchomvu huku Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akiiwakilisha serikali. Kiasi hicho cha fedha ndicho kilichoainishwa katika bajeti ya mwaka huu. Katika hafla fupi ya kusaini mkataba huo, Waziri Mkuya alisema, "TRA haina budi kuwatengenezea wafanyakazi wake mazingira mazuri yatakayowafanya wajitume kukusanya kodi na kukataa rushwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako