• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi aeleza umuhimu wa utafiti kuhusu nafasi ya China kwenye Vita Kuu ya Pili ya Dunia

    (GMT+08:00) 2015-07-31 19:31:57

    Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kufanyika juhudi zaidi katika kutafiti vita ya China dhidi ya uvamizi wa Japan na nafasi yake katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

    Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesema hayo kwenye semina ya mafunzo iliyohudhuriwa na wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China iliyofanyika jana. Amesema China ingependa kuonyesha uamuzi wake thabiti wa kulinda matunda ya ushindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na pia usawa na haki ya utaratibu wa kimataifa. Rais Xi amesema China itaheshimu historia, haitasahau mambo yaliyopita, itathamini amani na kuangalia mbele.

    Huu ni Mwaka wa 70 tangu ushindi wa watu wa China dhidi ya uvamizi wa Japan na kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako