• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la viwanda vya uhandishi lawatajirisha watibet

    (GMT+08:00) 2015-08-26 10:11:06


     

    Eneo la viwanda vya uhandisi la kabila la Tibet la wilaya ya Bailang lilianzishwa mwaka 2005, ni mradi uliojengwa kwa msaada wa mkoa wa Shandong. Tangu mkoa unaojiendesha wa Tibet ulipoanzishwa miaka 50 iliyopita, serikali kuu ya China imetunga sera na hutua nafuu mfululizo ili kuharakisha maendeleo ya mkoa huo. Mwenyekiti wa mkoa unaojiendesha wa Tibet Bw. Luosang Jiangcun amesema,

    "Tangu miaka 50 iliyopita, kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali zinawafuatilia sana maendeleo ya watu wa Tibet, na wananchi wote wametoa msaada kwa maendeleo ya Tibet, na wametuunga mkono kwa pande za watu, vitu na fedha."

    Eneo la viwanda vya uhadishi la kabila la Tibet la wilaya ya Bailang ni moja ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na sera nafuu na msaada mkubwa. Eneo hilo linaonesha umuhimu katika kuendeleza viwanda vya jadi vya watu wa kabila la Tibet, kuhimiza maendeleo ya uchumi wa wilaya na kuongeza mapato ya watu. Hivi sasa kuna viwanda vinane kwenye eneo hilo vkikiwemo kiwanda cha ufumaji cha Qiazhu, kiwanda cha magodoro cha Wangdan, kiwango cha uchoraji wa picha za Thang-ga na kiwanda cha samani za kitibet. Mkurugenzi wa kiwanda cha ufumaji cha Qiazhu Bi. Qu Zhen amesema, mwaka 1999 alianzisha kiwanda hicho kwa kutumia yuan elfu 6, baada ya juhudi za miaka mingi, idadi ya bidhaa zinazouzwa na kiwanda hicho inaongezeka siku hadi siku. Baada ya kuanzishwa kwa eneo la viwanda vya uhandisi la Bailang, imehamishia kiwanda chake kwenye eneo hilo. Hivi sasa kiwanda hicho kina wafanyakazi rasmi 45, na wengine zaidi ya 300 waliopata mafunzo wanafanya kazi nyumbani. Bidhaa za kiwanda hicho si kama tu zinauzwa mkoani Tibet, bali pia zinauzwa kwenye nchi nyingine zikiwemo India na Nepal, na zinapendwa sana na wateja. Kila mwaka kiwanda hicho kinaweza kupata faida yuan milioni moja. Chini ya uungaji mkono kutoka serikali na jitihada alizofanya, maisha ya Bi. Qu Zhen yamebadilika sana. Anasema,

    "Tangu nilipohamia kwenye eneo la viwanda vya uhandisi, nimejifunza mambo mengi kuliko zamani. Hapa ni tofauti sana na kijijini nilikoishi hapo awali. Hivi sasa mapato yetu yameongezeka, na aina ya bidhaa pia zimeongezeka kwa kiasi kikubwa."

    Kuongezeka kwa faida ya kiwanda cha ufumaji kumeleta maslahi halisi kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho. Bi. Ciqiong ni mwanamke wa kawaida wa wilaya ya Bailang, ambaye ana watoto wawili. Tangu alipoingia kwenye eneo la viwanda vya uhandisi na kuajiriwa na kiwanda hicho baada ya kupewa mafunzo, mapato yake yameongezeka na hivyo maisha ya familia yake na hali ya elimu ya watoto wake zimeboreshwa sana. Anasema,

    "Zamani nilishindwa kuendelea na masomo kwenye shule ya juu, wakati ule nilikuwa nyumbani na sikuweza kupata ajira. Maisha yalikuwa magumu sana. Kwenye muda wa mwanzo tangu nilipojiunga na kiwanda hicho, nilikuwa siwezi kufanya kazi yoyote. Lakini walimu wa hapa wamenifundisha ufumaji. Hivi sasa maisha ya familia yangu yameboreshwa sana. Kila mwezi naweza kupata yuan elfu 3 hadi 4. Hapo awali nilikuwa sina pesa, sikuweza kununua nguo nzuri za watoto hata kama nilikuwa naziona. Hivi sasa naweza kununua chochote nipendacho."

    Ingawa hali ya kiwanda inakuwa nzuri siku hadi siku, lakini mkurugenzi wa kiwanda hicho Bi. Qu Zhen hajawasahau watu wengine maskini. Kila mwaka kiwanda chake kinatoa mafunzo kwa wakulima kwenye eneo la viwanda vya uhandisi, ili waweze kufuma nyumbani na kupata mapato zaidi wakiwa na nafasi, ambapo hawashughuliki na mambo ya kilimo. Aidha ametenga asilimia 30 ya faida ya kampuni yake kwa ajili ya kupunguza umaskini. Anasema,

    "Serikali imetupatia msaada mkubwa, kwa hiyo siwezi kusahau uungaji mkono wa serikali. Hivi sasa asilimia 70 ya faida ya mwaka itatumika kwenye utengenezaji, na asilimia 30 ya faida ya mwaka itatumika kuwasaidia watu maskini. Nina matumaini kuwa ninaweza kuwaongoza watu wengine kujiendeleza kwa pamoja."

    Kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa sekta ya uhandisi, mwaka huu ukubwa wa thamani ya uzalishaji ya sekta ya uhandisi kwenye thamani ya uzalishaji ya wilaya kote umeongezeka kwa asilimia 10. Mkurugenzi wa idara ya biashara ya wilaya ya Bailang amesema, serikali ya huko imechukua hatua nyingi ili kuhimiza maendeleo ya sekta ya uhandisi. Anasema,

    "Serikali yetu inavihimiza viwanda viandae mafunzo ya ndani, na serikali inaviunga mkono. Tulitoa maombi ya miradi kwa idara husika za usimamizi, na kuviunga mkono viwanda hivyo. Tumealika watu wenye ujuzi na uzoefu kutoa mafunzo kwa wafanyakazi, kwa mfano wa mkurugenzi wa kiwanda cha magodoro cha Wangdan, yeye ni mwalimu hodari kwenye uhandisi."

    Kiwanda cha magodoro cha Wangdan kiliingia kwenye eneo la viwanda vya uhandisi mwaka 2013. hivi sasa magodoro yanayotengenezwa na kiwanda hicho yanauzwa kwa mahekalu ya ndani na nje ya nchi, kila mwaka kinaweza kuuza magodoro zaidi ya 600. Mapato ya mfanyakazi kwa mwezi yamezidi yuan 3000, na kila mwisho wa mwaka wafanyakazi wanaweza kupata bonasi, kiwango cha maisha yao kimeinuka kwa kiasi kikubwa.

    Wakati faida ya eneo la viwanda vya uhandisi inapoongezeka, ndipo maisha ya watu yanapoboreshwa, viwanda vya eneo hilo vinashikilia kanuni ya uzalishaji ya maendeleo endelevu, kutotumia mashine yoyote inayochufua mazingira. Vinatumia nyenzo za asili, na kutilia maanani uwiano kati ya uzalishaji na mazingira. Mkurugenzi wa kiwanda cha magodoro cha Wangdan Bw. Daping amesema,

    "Utengenezaji wa magodoro ya Wangdan umekuwa na historia ya miaka zaidi ya 1000. Nilipoanza kujifunza uhadisi huo, mwalimu wangu alinitaka nijifunze vizuri na kurithi. Lazima tutumie rangi za asili, na hatutatumia rangi zenye kemikali. Ingawa tunatumia rangi za asili, baada ya kutumia sisi lazima tufukie takataka zilizosababishwa na uzalishaji, na hatuwezi kuharibu mazingira."

    Kutokana na jitihada za watu wa Tibet, eneo la viwanda vya uhandisi limepata maendeleo makubwa, na limejenga njia moja ya kuwaendeleza watu wa huko. Mkurugenzi wa idara ya biashara ya wilaya ya Bailang ana imani kubwa kuhusu mpango wa maendeleo ya eneo hilo katika siku za baadaye. Anasema,

    "Kwanza, tutainua kiwango cha huduma cha eneo letu, na kuunda kamati ya usimamizi ya eneo. Pili tutaongeza nguvu za kuunga mkono viwanda. Tatu, tutatoa yuan milioni 2 katika kuboresha mazingira ya eneo. Nne, kwa kupita maendeleo ya eneo letu, tutaongoza maendeleo ya sekta ya uhandisi ya kabila la Tibet ya vijiji na wilaya za jirani. "

    Eneo la viwanda vya uhandisi la kabila la Tibet la Bailang ni mfano mdogo wa maeneo mengi ya viwanda mkoani Tibet, ambalo linawakilisha hali halisi ya maendeleo ya baadhi ya viwanda vidogo. Tangu miaka 50 iliyopita, watu wa Tibet wamefanya juhudi ili kujieletea maendeleo na kuondokana na umaskini, na kutimiza uwiano kati ya uchumi na mazingira. Wachina wana imani kuwa Tibet itafungliwa zaidi, na maisha ya watibet yatakuwa bora zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako