• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing ya mwaka 2015

    (GMT+08:00) 2015-08-28 15:54:10

    Msikilizaji mpendwa, karibu katika kipindi cha utamaduni wetu. Maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing yanafanyika kuanzia Jumatano hadi Jumapili wiki hapa Beijing. Mashirika 2,270 kutoka nchi na sehemu 82 yanashiriki kwenye maonesho hayo, ambayo ni maonesho makubwa ya pili duniani.

     


    Ufunguzi wa maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing ya mwaka 2015 yalifanyika Jumatano asubuhi. Kwa kuitikia mwamko wa kujenga "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya Baharini ya karne 21", ukumbi maalumu umeandaliwa kwa ajili ya mashairika ya uchapishaji kutoka nchi za njia ya Hariri zikiwemo Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Misri, Uturuki, India, Sri Lanka na Kazakhstan, ambayo yanaonesha vitabu, michoro, vitu vya sanaa katika maonesho hayo yatakayodumu kwa siku tano. Mashirika hayo pia yatafanya maonesho ya kuimba na kucheza ngoma na ya nguo za kijadi, ili kutangaza utamaduni wa nchi zao. Mbali na hayo, mashirika hayo yatasaini makubaliano ya ushirikiano na mashirika ya uchapishaji ya China.

    Hayo ni maonesho ya 22 ya vitabu ya Beijing, na mwaka huu nchi ya heshimu ni Falme za Kiarabu. Katika ufunguzi wa maonesho hayo, ngoma iliyochezwa na wasanii kutoka nchi hiyo inawavutia watazamaji wengi. Naibu waziri wa utamaduni, vijana na maendeleo ya jamii wa nchi hiyo Bibi Afra Muhamed Sabir anaongoza ujumbe wa watu kutoka mashirika 41 maarufu ya uchapishaji kushiriki kwenye maonesho hayo, na kibanda chao chenye eneo la mita 1,000 za mraba kimepambwa kwa mtindo wa kiarabu. Bibi Afra anasema, China na nchi za kiarabu zote ni nchi zenye historia ndefu na utamaduni unaong'ara, kufuatia mawasiliano ya biashara kuongezeka siku hadi siku, mawasiliano ya utamaduni yanaonesha umuhimu wake.

    "Kufuatia vitabu vingi vizuri vya China kuuzwa katika nchi za nje, wasomaji wengi zaidi wa nchi za kiarabu wanavutiwa zaidi na utamaduni wa China. Tunapenda sana kufanya mawasiliano na ushirikiano na China, na kujenga Njia mpya ya Hariri ya sekta ya uchapishaji. "

    Ili kuwafahamisha wasomaji wengi zaidi kuhusu utamaduni wa kiarabu, Falme za Kiarabu pia imetenga eneo maalum la mchezo, na kuwaalika wasanii maarufu wa maandishi ya kiarabu kumpatia kila msomaji wa China anayeshiriki kwenye mchezo jina moja la kiarabu, na kumzawadia karatasi ya maandishi ya kiarabu ya jina hilo. Li Hui ni msichana aliyepata zawadi ya maandishi ya kiarabu, anafurahi kupata zawadi hiyo.

    "Unaandika matamshi ya jina lako la kichina, halafu msanii analitafsiri kwa kiarabu kutokana na matamshi hayo. Hilo ni jina langu la kiarabu, naitwa Li Hui. Naona maandishi ya jina la rafiki yangu yanaonekana kama ua, na langu kama moto. Kila neno wanaloandika ni tofauti na la kichina, lakini umbo lake ni zuri sana. Nataka kujifunza, lakini naona ni ngumu sana."

    Licha ya hayo, Falme za Kiarabu pia imewaalika wachoraji Hina maarufu kushiriki kwenye maonesho hayo. Bibi Zhang Xinling naye anapata kuchorwa Hina.

    "Maana yake ni "Nakupenda." Naipenda sana. Baada ya hina kukauka, itadumu kwa muda. Ukilinganishwa na mchoro wa jadi wa China, mchoro huu wa hina una sifa pekee."

    Saudi Arabia inayohudhuria maonesho hayo kwa miaka mitano mfululizo, mwaka huu sio tu imeleta vitabu vipya zaidi ya aina ya 700 vinavyohusiana na sekta mbalimbali za Saudi Arabia, bali pia imejenga maeneo kadhaa ya utamaduni, ili kuwaonesha watazamaji utamaduni na sanaa ya Saudi Arabia. Naibu mkuu wa idara ya ushirkiano wa kimataifa ya wizara ya elimu ya juu ya nchi hiyo Walid anasema,

    "Tuna methali isemayo: Tafuta Elimu, hata kama ni Uchina. Saudi Arabia na China sio tu lulu mbili zinazong'ara katika njia ya Hariri ya kale, bali pia zinatoa mchango mkubwa katika njia mpya ya Hariri. Tangu tuanze kushiriki kwenye maonesho ya vitabu ya Beijing, tumewashirikisha wakalimani wazuri wa China kutafsiri vitabu zaidi ya 50 kuhusu utamaduni na historia ya Saudi Arabia, tunataka kuwafahamisha wasomaji wa China utamaduni mwingi zaidi wa kiarabu, ili wapate machaguo mengi kuhusu dunia hiyo kubwa yenye tamaduni za aina mbalimbali."

    Asante sana Ronald kwa ripoti yako. Msikilizaji mpendwa, baada ya kusikiliza maelezo kuhusu maonesho ya vitabu ya Beijing, sasa nitawaelezea kuhusu baadhi ya maonesha makuu ya vitabu duniani.

    Maonesho ya kimataifa ya vitabu ya Beijing yalizinduliwa mwaka 1986. Kila mwaka mashirika zaidi ya 500 ya uchapishaji ya China na mashirika mengine zaidi ya 2000 kutoka nchi na sehemu 80 yanakuja kuhudhuria maonesho hayo, idadi ya watazamaji inafikia laki 2 hivi. Hivi sasa Maonesho ya kimataifa ya Beijing, Maonesho ya vitabu ya Frankfurt, Maonesho ya vitabu vya London na maonesho ya vitabu ya Marekani yanasifiwa kama maonesho bora manne ya kimataifa ya vitabu.

    Maonesho ya vitabu ya Marekani yalizinduliwa mwaka 1947, mpaka sasa maonesho hayo yamekuwa na historia ya miaka 68. Maonesho hayo yalizinduliwa na shirikisho la wafanyabiashara wa vitabu la Marekani ABA pamoja na Shirikisho la uchapishaji la Marekani AAP, ambayo yalikuwa maonesho ya manunuzi ya vitabu kwa wafanyabiashara wa vitabu yaliyoandaliwa na mashirika ya uchapishaji ya Marekani. Baada ya maendeleo ya miaka mingi, maonesho hayo yamekuwa makubwa na yenye uwezo wa kujadili kuhusu manunuzi ya vitabu na haki ya kunakili vitabu ambayo yanashirikisha nchi zote zinazozungumza lugha ya Kingereza.

    Maonesho ya vitabu ya Marekani yanasifiwa kama shughuli kubwa zaidi inayoonesha vitabu vya Kingereza duniani, ambayo pia ni pahali pakubwa zaidi pa biashara ya vitabu. Kila ifikapo mwezi Mei na Juni, maonesho hayo hufanyika katika miji mbalimbali ya Marekani ikiwemo New York, Washington, Chicago na Los Angeles. Licha ya kuonesha vitabu, maonesho hayo pia yanaandaa kongamano, maonesho madogomadogo, semina na ukumbi wa utamaduni. Shughuli ya biashara ya haki ya kunakili pia inachukua nafasi kubwa katika maonesho hayo, kila mwaka wafanyabiashara wa vitabu, mameneja wa uchapishaji na wataaluma wa haki za kunakili katika kituo cha haki za kunakili hujadili kuhusu kununua kazi za fasihi au haki za kunakili vitabu.

    Soko la vitabu la Marekani ni soko kubwa zaidi la vitabu duniani, na kila mwaka maonesho ya vitabu ya Marekani yanawavutia wahusika wengi wa mashirika zaidi ya elfu moja ya uchapishaji kutoka nchi na sehemu zaidi ya 80 duniani. Maonesho ya vitabu ya Marekani yanachukuliwa kama moja ya maonesho muhimu zaidi ya vitabu vya kiingereza duniani, ambayo pia ni alama ya maendeleo ya shughuli ya uchapishaji ya kimataifa.

    Maonesho ya vitabu ya Leipzig ya Ujerumani yana historia ndefu. Imefahamika kwamba chanzo cha mtindo wa maonesho ya vitabu ya kimataifa ya kisasa ni urithi wa maonesho ya vitabu ya Leipzig ya Ujerumani yaliyozinduliwa mwanzoni mwa karne ya 19. Maonesho hayo yanayoandaliwa na kampuni ya maonesho ya Leipzig ya Ujerumani kila inapofika mwezi Machi na Aprili yanafanyika katika kituo cha maonesho ya Lepizig nchini Ujerumani, ambayo ni tukio muhimu katika shughuli ya uchapishaji wa vitabu katika eneo linalotumia lugha ya Kijerumani. Maonesho hayo yanawajengea watu jukwaa la biashara ya vitabu vipya , ambalo wafanyabishara ya vitabu, wasomaji na vyombo vya habari wanaweza kuwasiliana moja kwa moja.

    Kuanzia karne ya 18, Leipzig ilikuwa kituo cha utamaduni cha Ujerumani, ambacho kilijumuisha mashirika muhimu ya uchapishaji ya Ujerumani na kuwa makao makuu ya uchapishaji. Mwaka 1948 Leipzig ilifanikiwa kufanya maonesho ya vitabu, ambayo yalikuwa sehemu ya maonesho ya viwanda. Maonesho hayo yameendelea kutoka maonesho ya ngazi ya taifa hadi maonesho ya eneo la Ulaya, na mwishoni yamekuwa maonesho muhimu ya kimataifa.

    Katika miaka kumi iliyopita, maonesho hayo yalipata maendeleo makubwa, ambayo yamekuwa maonesho ya kimataifa yanayoshirikisha shughuli ya vitabu, shughuli ya uchapishaji, usimamizi wa maktaba na shughuli ya vitabu vya kale. Mbali na hayo, maonesho hayo yanatilia maanani vitendo vya kusoma vya vijana, ambayo yanafanya juhudi ya kuwafanya vijana wawe na hamu ya kuvipenda vitabu na kujibu mara moja mahitaji ya vijana.

    Maonesho ya vitabu ya Frankfurt Ujerumani ni maonesho makubwa zaidi ya vitabu dhuniani, ambayo yanasifiwa kama "Michezo ya Olimpiki ya wachapishaji duniani". Maonesho hayo yanaandaliwa na kampuni ya maonesho ya Frankfurt AuM ya shirikisho la uchapishaji na wafanyabiashara wa Ujerumani. Maonesho hayo yanatoa fursa kwa wachapishaji, wawakilishi na wafanyakazi wa maktaba kujadili kuhusu biashara ya haki ya kunakili, shughuli ya uchapishaji, na maagizo ya vitabu. Maonesho hayo yalizinduliwa mwaka 1949 na shirikisho la vitabu la Ujerumani, na lengo lake ni kuyaruhusu mashirika yoyote ya uchapishaji duniani kuonesha kitabu cha aina yoyote. Baada ya kufanya kwa awamu zaidi ya 60, uwezo mkuu wa maonesho ya Frankfurt ni kusukuma mbele biashara ya haki ya kunakili. Takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka zaidi ya asilimia 75 ya biashara ya haki za kunakili duniani imemalizwa katika maonesho ya vitabu. Kwa upande mmoja, watu husika wanaoshughulikia haki za kunakili wa mashirika ya uchapishaji wanakuja kununua haki ya kunakili katika nchi za nje au haki za kutafsiri, kwa upande mwingine wawakilishi wa wanafasihi wanatafuta kampuni ya uchapishaji kutoka nchi za nje. Katika maonesho ya vitabu ya Frankfurt ya mwaka jana, mashirika 8,008 kutoka nchi 100 yalishiriki maonesho hayo, yakiwemo mashiriki 4,900 hivi ya kimatafa. Aidha, maonesho hayo pia yanawavutia watazamaji 40,000 wa sekta ya uchapishaji.

    Maonesho ya vitabu ya Paris

    Maonesho ya vitabu ya Paris yalizinduliwa mwaka 1984 na shirikisho la uchapishaji la Ufaransa, ambayo ni moja kati ya shughuli muhimu ya utamaduni ya Ulaya. Maonesho hayo kila mwaka yanayashirikisha mashirika zaidi ya elfu moja ya uchapishaji kutoka nchi mbalimbali duniani. Maonesho ya vitabu ya Paris ya mwaka 2015 yalifanyika tarehe 20 hadi 23 Machi katika kituo cha maonesho cha Versailles cha Paris, na kuchukua nafasi ya eneo la mita elfu 40 za mraba, mashirika 1,200 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 50 yalikwenda kushiriki maonesho hayo. Tofauti na maonesho mengine, maonesho ya vitabu ya Paris yanatoa wito kwa mara ya kwanza kuwa kila awamu ya maonesho sio tu itaweka mada kuu ya fasihi ya kigeni, bali pia itafuatilia utamaduni na fasihi ya mji mkubwa. Katika maonesho ya vitabu ya Paris ya mwaka 2015, Brazil imekuwa nchi ya heshima ya maonesho hayo. Mbali na hayo, maonesho hayo pia yaliialika miji miwili kuwa miji ya heshima ambayo ni Krakow na Wroclaw ya Poland, ili kuwafahamisha wasomaji maendeleo mapya ya fasihi ya Poland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako