• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya maiti 70 za wahamiaji zapatikana ndani ya lori katika barabara kuu ya Austria

    (GMT+08:00) 2015-08-28 18:09:53

    Wizara ya mambo ya ndani ya Austria imesema idadi ya maiti zilizokutwa ndani ya lori lililotelekezwa nchini Austria imezidi 70 kutoka kadirio la mwanzo la kati ya 20 hadi 50.

    Lori hilo linalomilikiwa na raia wa Romania na lenye nambari za usajili za Hungary, liligunduliwa jana kwenye barabara kuu ya jimbo la Burgenland, mashariki mwa Austria. Polisi wa Austria wanashirikiana na wa Hungary kutafuta taarifa muhimu kuhusu watu hao kupitia mtandao wa Internet.

    Wakati tukio hilo linatokea, viongozi wa nchi za Ulaya walikutana mjini Vienna, na kujadili kwa kina suala la kuwapokea wakimbizi. Afisa wa Austria aliyehudhuria mkutano huo amesema watu wanaosafirisha wahamiaji hao wanatakiwa kuwajibika kwa tukio hilo la ukatili dhidi ya binadamu.

    Habari pia zinasema boti mbili zilizobeba wahamiaji zimepinduka jana katika pwani ya Libya, na wakimbizi 200 kati ya 500 waliokuwemo kwenye boti hizo wameokolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako