• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping akutana mshauri wa rais wa Marekani kuhusu suala la usalama Bibi Susan Rice

    (GMT+08:00) 2015-08-29 19:25:15

    Rais Xi Jinping wa China jana amekutana na mshauri wa rais wa Marekani kuhusu suala la usalama Bibi Susan Rice ambaye yuko ziarani mjini Beijing.

    Rais Xi Jinping amesema kutokana na mwaliko wa rais Barack Obama wa Marekani, atafanya ziara nchini Marekani mwezi ujao. Amesema kuwa anapenda kubadilishana maoni na rais Obama kuhusu masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili, kuzungumzia mpango wa kuzidisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili na kuhimiza ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili, na kuleta maslahi mengi zaidi kwa ajili ya watu wa nchi hizo mbili na dunia nzima.

    Ziara hiyo ya Rice ni kufanya maandalizi kwa ajili ya ziara ya rais Xi Jinping nchini Marekani mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako