• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Omar Al Bashir wa Sudan anakuja China kuhudhuria maadhimisho ya ushindi wa vita dhidi ya ufashisti

    (GMT+08:00) 2015-08-31 10:08:08

    Rais Omar al Bashir wa Sudan anatarajiwa kuja China Beijing kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan, Ali Al Saddiq amesema katika ziara yake ya siku nne, rais Bashir atashiriki kwenye sherehe za China za maadhimisho ya ushindi dhidi ya ufashisti, na na pia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili.

    Wakati huohuo waziri wa usafiri na barabara wa Sudan Makkawi Mohammed Ahmed amesema rais Al Bashir atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali ya Sudan na kampuni ya China kwa ajili ya ujenzi wa kilomita elfu moja za reli mashariki mwa Sudan kwa gharama ya dola bilioni 1.4. Pia atashuhudia kusainiwa makubaliano ya ununuzi wa ndege mbili na meli 9 za kusafiri kwa njia ya mto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako