• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha kauli ya kushindwa kwa mkakati wa kufufua mikoa ya Kaskazini Mashariki

    (GMT+08:00) 2015-08-31 18:08:21

    Ofisa wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China leo hapa Beijing amesema, kauli kuhusu kushindwa kwa mkakati wa kufufua mikoa ya Kaskazini Mashariki haiendani na hali halisi. Amesema kutokana na makadirio, katika nusu ya pili ya mwaka huu, uchumi wa mikoa mitatu iliyopo Kaskazini Mashariki ya China utatulia, na huenda ukawa na ongezeko. 

    Watu zaidi ya milioni 100 wanaishi katika sehemu ya Kaskazini Mashariki ya China inayochukua moja kati ya saba ya eneo la ardhi ya China. Kuanzia mwaka jana, uchumi wa sehemu hiyo ulikumbwa na changamoto kubwa, ikiwemo kushuka kwa ongezeko la uchumi, baadhi ya sekta na makampuni yalikabiliwa na shida kubwa za kuendelea na shughuli zake, na serikali ya mikoa kushindwa kudumisha uwiano kati ya mapato na matumizi ya fedha. Kutokana na hali hiyo, msemaji wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Li Puming amezungumzia hali hiyo alijumuisha hali ya kiuchumi ya mikoa mitatu iliyopo sehemu ya Kaskazini Mashariki, akisema,

    "katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ongezeko la uchumi la mikoa ya Liaoning, Jilin na Heilongjiang lilikuwa asilimia 2.6, asilimia 6.1 na asilimia 5.1. Mikoa hiyo ina shinikizo kubwa la kushuka kwa ongezeko la uchumi. Ongezeko la jumla la mapato ya taifa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu lilikuwa asilimia 7. Na ongezeko hilo katika mikoa hiyo mitatu lilikuwa la chini kuliko kiwango cha nchi nzima."

    Kutokana na kauli kuhusu kushindwa kwa mkakati wa kufufua mikoa ya Kaskazini Mashariki, Bw. Li amesema

    "Sikubaliani na kauli hiyo. Kuanzia mwaka 2003, kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali ya China wametoa uamuzi wa kufufua mikoa ya Kaskazini Mashariki, hatua na sera mbalimbali zimetolewa, maendeleo ya uchumi ya sehemu hiyo yameinuka na kufikia kiwango kipya, sekta ya uzalishaji wa vifaa na sekta nyingine zenye nguvu ya ushindani zimeinuka, uzalishaji wa makampuni umeboreshwa sana, na kilimo cha kisasa, ujenzi wa mfumo wa uhakikisho ya kijamii, mageuzi ya miundo ya miji na ukarabati wa makazi duni pia vimepata maendeleo makubwa."

    Mwezi Agosti mwaka jana baraza la serikali la China lilitoa hatua za kuunga mkono kufufua mikoa ya Kaskazini Mashariki. Bw. Li Pumin amesema, hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu, miradi 80 inatekelezwa na mingine imekamilika, na uwekezaji umefikia Yuan bilioni 567.6, hayo yameweka msingi kwa maendeleo na ustawi wa sehemu za Kaskazini Mashariki mwa China. Amekadiria kuwa, uchumi wa sehemu hiyo katika nusu ya pili ya mwaka huu utatulia na kuwa mzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako