• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 16 wapitishwa kugombea urais nchini Burkina Faso

    (GMT+08:00) 2015-08-31 18:09:24

    Baraza la katiba la Burkina Faso limepitisha orodha ya majina 16 kati 22 watakaogombea nafasi ya urais katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 11 mwaka huu nchini humo.

    Kati ya wagombea hao, wawili ni wanawake, na hii ni mara ya kwanza kwa wanawake kupitishwa kugombea nafasi ya urais nchini Burkina Faso. Majina ya wagombea wengine 6, wakiwemo wawili ambao walikuwa karibu na rais wa zamani wa nchi hiyo Blaise Compaore, yalikataliwa. Wengine ambao wamekataliwa kugombea nafasi hiyo ni wagombea binafsi ambao hawakufanikiwa kulipia dhamana ya dola za kimarekani 41,000 au hawakuwasilisha vielelezo vilivyotakiwa.

    Madai yoyote kuhusiana na orodha ya wagombea yatashughulikiwa na Baraza la Katiba hadi Septemba 9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako