• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nafasi ya mwanamke kwenye sekta ya habari Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2015-09-14 09:18:40

    Katika kipindi cha leo, mwenzangu Caroline Nassoro alipata fursa ya kuwahoji wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania kuhusu nafasi ya mwanamke katika tasnia ya habari. Wanahabari hao Bi. Moza Saleh kutoka Hits FM Zanzibar, Khadija Khalili kutoka gazeti la Tanzania Daima, na Mwasu Sware kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC, walikuja hapa China kwa ziara fupi ya mafunzo. Na kutokana na kuwa, wanahabari wote waliokuja kwenye ziara hiyo ni wanawake, Carol alitaka kujua kama hiyo ni ishara kuwa, nafasi ya mwanamke kwenye tasnia ya habari imeanza kutambulika.

    Ukweli ni kwamba zama za wanawake kukaa nyumbani tu na kumtegemea mume kwa kila kitu zimepitwa na wakati. Mama na baba katika familia wanatakiwa kushirikiana pamoja katika kutunza familia. Ndio, hatukatai kuwa baba ni kichwa cha familia, lakini kama tunavyosema kwenye kipindi hiki, mama ni shingo, au ni waziri mkuu wa familia, hivyo wote wawili wanatakiwa kushirikiana pamoja ili kupunguza shinikizo la kutunza familia kwa baba peke yake. Kwa upande wa elimu, bado kuna familia ambazo mpaka leo zinatoa kipaumbele kwa mtoto wa kiume kuliko mtoto wa kike. Mwenzangu Carol alitaka kujua wanahabari hao wanatumiaje nafasi zao kuelimisha jamii kuhusu elimu kwa mtoto wa kike?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako