• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nafasi ya mwanamke katika jamii

    (GMT+08:00) 2015-09-21 18:27:57

    Katika kipindi cha Sauti ya Wanawake kinachokujia muda kama huu kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa. Katika kipindi hiki tunazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke na jamii kwa ujumla, changamoto anazokumbana nazo katika jitihada zake za kujikwamua kimaisha, na pia mafanikio ambayo yamepatikana katika suala zima la usawa wa jinsia.

    Nafasi ya mwanamke kwenye jamii ni suala ambalo linajadiliwa sana katika zama za sasa. Wengi wanasema haiwezekani kwa mwanamke na mwanaume kuwa sawa, na wengine wanasema inawezekana, wakimaanisha nafasi anazopewa mwanaume, mwanamke pia anaweza. Katika kipindi cha leo, mwenzangu Caroline Nassoro amepata firsa ya kuzungumza na wafanyakazi wa Shirika la Habari Zanzibar, ZBC, ambao ni Hasina Hamad Rajab huyu yuko ZBC upande wa Pemba, na Salma Abdallah Faraji, huyu ni ofisa raislimali watu kutoka ZBC Unguja. Wanaanza kwa kueleza nafasi ya mwanamke katika suala la elimu, uongozi, na hata siasa, hususan kwa upande wa Tanzania Visiwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako