• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwango kikubwa siku hadi siku cha kuvunja ndoa

    (GMT+08:00) 2015-10-05 15:06:47

    Katika kipindi cha leo tutazungumzia suala la ndoa na talaka. Kama utakumbuka Pili, kuna mkongwe mmoja wa muziki aliwahi kuimba kuwa 'Kuolewa ni jambo la sifa', na pale binti anapoolewa au kijana anapooa, wazazi, ndugu, na jamaa wanaona fahari sana kwani ni hatua muhimu katika maisha ya mwanadamu. Familia hutumia miezi kadhaa au hata miaka kuandaa harusi, ili tu iwe ya kufana na kuvutia. Lakini sasa, idadi ya ndoa zinazovunjika inaongezeka kwa kasi duniani.

    Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa, nchi inayoongoza kwa idadi kubwa ya talaka duniani ni Belgium, ambayo ina asilimia 71, na Marekani ina asilimia 53 ya talaka. Lakini kama ulivyosema Carol, kuoa au kuolewa ni jambo jema, na takwimu zilizotolewa hivi karibuni na wizara ya mambo ya jamii ya China zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, wapenzi wapatao milioni 6.2 waliandikisha ndoa kote nchini China, huku idadi ya wale waliovunja ndoa ilifika milioni 1.51, ambazo ni 4.1:1, kiwango ambacho kilikuwa 4.8:1 mwaka jana.

    Profesa Zhou Xiaozheng wa Chuo Kikuu cha Renmin cha China anasema, suala la talaka linagusa jamii nzima, na hii ni mara ya tatu kuwa na kiasi kikubwa cha ndoa zinazovunjika tangu kuanzishwa kwa taifa la China, na pia linasababishwa na mazingira mapya ya jamii haswa katika miaka ya karibuni. Bibi Liu mwenye umri wa miaka 35 anafanya kazi katika serikali ya mtaa mjini Taiyuan mkoani Shanxi. Mwaka mmoja uliopita, alitalikiana na mumewe. Sasa ilikuwaje mpaka akaolewa? Bibi Liu alipofikisha miaka 32 na bado hajaolewa, ndugu, jamaa na marafiki wake wakamhimiza afunge ndoa, naye ili kuwaridhisha, akafunga ndoa haraka. Pili kama unavyojua, uchumba ni tofauti na ndoa, na hawa watu hawakujuana vizuri kabla ya kuoana, kinachofuata baada ya ndoa ni ugomvi kila kukicha na mumewe, mwisho wa yote, mumewe akpata mchepuko, na Bi Liu alipofahamu, aliamua kumpa talaka mumewe.

    Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha ndoa kuvunjika. Sababu ya Bi Liu ni moja, lakini kuna wale wanaooana ili tu na wao waonekane wameoa/wameolewa, lakini hakuna mapenzi kati yao, kuna wanaooana kutokana na maslahi, na sababu nyingine kadha wa kadha. Sasa Mkuu wa mhakama wa Dongtaipu mjini Taiyuan Bibi Cao Liyin anakumbuka baadhi ya kesi za talaka alizoshughulikia. Anasema baadhi ya wapenzi wanafunga ndoa sio kutokana na mapenzi, bali ni malengo yao halisi, yakiwemo kutaka kubaki katika mji mkubwa, kujipatia ajira, ama kutokana na kuwa mpenzi wake ana nyumba. Ndoa nyingi zinazovunjika ni za vijana waliozaliwa baada ya miaka ya 1980.

    Mfano wa ndoa iliyovunjika kutokana na tofauti za kimaisha ni ile ya Bibi Zhang mwneye umri wa miaka 30. Binti huyu alizaliwa katika familia tajiri, hivyo siku zote ameishi maisha ya kifahari, sasa akaolewa na mwanaume ambaye hali yake kimaisha si ya juu kama yake. Pili unajua kwa kawaida mwanaume anapenda kumhudumia mke wake au sio? Lakini kwa kijana huyu, ilibidi aishi na familia ya mkewe, sasa ukizingatia kuwa yeye si tajiri, ni wazi kuwa maisha kwenye nyumba hiyo yatamshinda. Basi kijana akaanza kutoa visingizio kuwa anafanya kazi za ziada, hivyo akawa anarudi nyumbani mara chache sana kadri siku zinavyoenda, mwisho wa yote wakaamua kuvunja ndoa.

    Hali hii inawatokea vijana wengi. Kama tulivyosema kuwa vijana wengi wa miaka ya 1980 ndio wanashindwa kudumu katika ndoa zao, na hii inatokana na kudekezwa sana na wazazi wao, hivyo hawana uelewa wowote wa kujenga uhusiano, na kama msuguano kidogo ukitokea, uamuzi wao wa haraka ni kuvunja ndoa. Lakini kama hii itakuwa chaguo la kwanza la kutatua mzozo katika ndoa, wengi wanaweza kuiga tabia hiyo, na hivyo kufanya watu wengine kukosa uaminifu na ndoa.

    Kuna baadhi ya watu huwa wanasema heri niwe peke yangu kuliko kupitia kadhia ya talaka. Mara nyingi mhariri wa gazeti la "Wanawake wa China" ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la mashaurinao ya kisiasa la umma la China Bibi Shang Shaohua anatoa wito wa kuweka kipindi cha miezi 3 hadi 6, ili wanandoa waweza kutulia na kufikiria tena baada ya kukidhi ombi la kuvunja ndoa yao. Hivi sasa mijini Hangzhou, Guangzhou, Shenzhen, Qingdao na Lanzhou nchini China, wanandoa wanaotaka kutalikiana wanapaswa kufanya miadi kwa wiki moja hadi mbili. Kutokana na kukutana na kuzungumza kwa kina, wanandoa wengi walifuta maombi yao ya talaka na wanaendelea na ndoa zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako