• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya 18 ya vitabu ya kimataifa ya Nairobi yafanyika

    (GMT+08:00) 2015-09-25 10:24:12

    Maonesho ya 18 ya vitabu ya kimataifa ya Nairobi yanafanyika kuanzia Jumatano wiki hii hadi Jumapili kwenye jumba la maonesho la Sarit Center jijini Nairobi.

    Kauli mbiu ya maonesho hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la uchapishaji la Kenya ni "Twende Digital". Katika zama za leo, Digital ikiwa ni mwelekeo wa kisasa, imeibua mageuzi makubwa kwenye sekta zote zinazohusiana na mawasiliano na upashanaji habari, ikiwemo uchapishaji vitabu. Kwa sekta hiyo, digital si kama tu ni changamoto, bali pia ni fursa. Na namna ya kukabiliana na suala hilo inaamua mustakbali wa sekta hiyo nzima.

    Vitabu, vya kubuni au vyenye hadithi za hali halisi ni kioo cha jamii wanazotoka waandishi. Kwa hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kwamba jamii inaweza kuwasiliana vizuri kuhusu maswala yanayoikabili na kufanya hivyo kupitia vitabu ili kukuza amani miongoni mwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako