• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simu za mkononi za Huawei zinapendwa zaidi nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2015-10-08 08:50:57


     

    Nchini Zimbabwe bidhaa zilizotengenezwa na China zinapendwa sana na wananchi wa nchi hiyo, hasa simu za mkononi za Huawei. Mwaka 2012 simu za mkononi za Huawei zilianza kuuzwa nchini Zimbabwe, hivi sasa idadi ya uuzaji wa simu hizo imechukua nafasi ya tatu sokoni baada ya Nokia na Samsung, na katika soko la simu za kisasa nchini humo, idadi ya uuzaji wa simu za mkononi za Huawei imezidi simu za mkononi za Apple.

    Nchini Zimbabwe kila sehemu ambapo simu za mkononi zinauzwa, simu za Huawei lazima zitakuwepo. Hivi sasa Huawei imekuwa chapa ya simu za mkononi inayopendwa zaidi na wazimbabwe badala ya Apple. Bibi Petunie aliwahi kuwa mpenzi wa simu za mkononi za Apple, lakini tangu alipotumia simu ya mkononi ya Huawei, alivutiwa sana na simu ya hiyo. Anasema,

    "Betri ya simu ya mkononi ya Huawei ni nzuri sana. Ni kawaida umeme kukatika mara kwa mara nchini Zimbabwe, hatuwezi kuchaji simu wakati wowote, natumai betri ya simu yangu inaweza kufanya kazi kwa siku moja. Baada ya kuchaji simu yangu asubuhi, naweza kuitumia hadi asubuhi ya siku ya pili, hivyo sina haja ya kuichaji mara kwa mara. "

    Ukweli ni kwamba, nchini Zimabawe kuna tatizo kubwa la mgao wa umeme, hivyo uwezo wa muda wa matumizi ya betri ni kigezo muhimu wakati watu wanapochagua simu za mkononi. Betri za simu za mkononi aina ya Apple na Samsung zinaweza kutumika kwa nusu siku hadi siku moja tu, lakini zile simu za Huawei huweza kutumika kwa siku moja na nusu. Licha ya hayo, kwa kulinganisha na simu za mkononi za chapa nyingine, bei ya simu za mkononi za Huawei ni nafuu sana, bei hizo zinaanzia dola za kimarekani 60 hadi 600, lakini uwezo wao haupungui kuliko simu za chapa nyingine. Hivyo simu za mkononi za Huawei zinapendwa zaidi na wazimbabwe walio na kipato cha wastani cha dola za kimarekani 300.

    Kampuni ya Huawei iliingia kwenye soko la Afrika mwaka 1998, na imefanya biashara nchini Zimbabwe kwa miaka 17. Hapo awali shughuli kuu ya kampuni ya Huawei nchini Zimbabwe ilikuwa ni kujenga mtandao wa Internet kwenye simu za mkononi. Baada ya mwaka 2012, kampuni hiyo iligundua kuwa soko la Afrika lina mahitaji makubwa kwa simu za mkononi za kisasa, hivyo ilianza kuingia kwa pande zote kwenye soko hilo. Maneja wa uhusiano na jamii wa kampuni ya Huawei nchini Zimbabwe Bw. Lai Cuihai anasema,

    "Nchi nyingine zilizoendelea duniani zimekamilisha mchakato wa matumizi ya simu za mkononi za kisasa kutoka simu za mkononi za kawaida, lakini Afrika bado iko kwenye mchakato huo. Watu wengi bado wanatumia simu za mkononi za kawaida, na simu za mkononi za kisasa zimechukua asilimia 10 hadi 15 tu kwenye soko la simu za mkononi, hii inaonesha mustakabali mzuri wa soko la Afrika kwa kampuni ya Huawei."

    Lakini jinsi ya kuingiza simu za mkononi za kisasa kwenye soko la Zimbabwe ni ngumu sana. Meneja Lai Cuihai alitambua kuwa si rahisi kueneza soko kwenye soko la simu za mkononi za kisasa lililotawaliwa na chapa za Apple na Samsung. Anasema,

    "Tunakabiliana na ushindani mkali kutoka Apple na Samsung kwenye soko la simu za mkononi za kisasa. Kampuni ya Huawei ina muda mfupi tangu iingie kwenye soko la simu za mkononi, na kwa kweli kwa upande wa athari ya chapa liko pengo kati ya Huawei na chapa za Apple na Samsung. Lakini baada ya maendeleo ya miaka ya karibuni, pengo hilo linapungua. Simu ya Mates iliyotolewa na kampuni yetu imefikia kiwango cha juu zaidi duniani katika umbile na uwezo. Licha ya hayo, tuliendesha mtandao wa mawasiliano ya simu kwa miaka mingi, hivyo ni rahisi zaidi kwa simu za mkononi za Huawei kuunganishwa na mtandano huo, mawimbi mazuri zaidi ni ubora moja wa simu za mkononi za Huawei. "

    Meneja Lai anasema, ili kuongeza athari ya chapa ya Huawei, kila mwaka kampuni ya Huawei inatumia asilimia 10 ya faida katika utafiti ili kuharakisha uvumbuzi wa teknolojia. Wakati huo huo kampuni ya Huawei imeanza kutilia maanani matangazo ya biashara duniani, hatua ambazo zimepongezwa sana na wazimbabwe.

    Ingawa kipato cha wazimbabwe si kikubwa, lakini wanapenda sana kufuata mitindo. Wanapenda soko, wanapenda kujipiga picha. Kwenye duka maalumu linalouza simu za mkononi za Huawei mjini Harare, Bibi. Retundo alikuwa anachagua simu moja ya Huawei. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, sababu yake ya kuchagua simu ile ni kuwa Huawei ni mfadhili wa klabu ya Arsenal, na simu hiyo inaweza kukidhi mahitaji yake ya kupiga picha. Anasema,

    "Mimi ni mpenzi wa timu ya Arsenal, najua simu za mkononi za Huawei ni mfadhili wa klabu ya Aseanal, hivyo naweza kupata habari yoyote kwa kupitia simu ya Huawei. Licha ya hayo, simu hiyo ina uwezo wa kuzuia kutetemeka wakati wa kupiga picha, hivyo inapiga picha nzuri sana."

    Mmiliki wa duka hilo Bw. Kariwo amesema, kila mwezi duka lake linaweza kuuza simu za mkononi za Huawei 1000 hivi. Kwa wateja ambao wanapenda simu za Huawei lakini hawana mapato makubwa, Bw. Karibo anawaruhusu walipe kwa awamu. Anasema,

    "Wanunuzi wengi wanalipa pesa taslimu, lakini baadhi ya kampuni zinalipa kwa siku saba. Hivi sasa tunazingatia njia ya kulipa kwa vipindi kadhaa. Tunafanya mazungumzo na baadhi ya benki na kampuni za mikopo, kama mteja akitaka kununua simu yetu, anaweza kutoa ombi kwa benki au kampuni za mikopo, kama ombi hilo likipitishwa, ataweza kupata pesa na kununua simu yetu, halafu atalipa mkopo kwa benki au kampuni za mikopo, hivyo duka letu halitaathirika. "

    Maneja wa simu za mkononi wa kampuni ya Huawei nchini Zimbabwe Bw. Yang Sen amejulisha kuwa hivi sasa bado hakuna duka maalumu linalouza simu za mkononi za Huawei nchini humo, na duka hilo bado ni la majaribio, lakini ufanisi ni mzuri. Kampuni ya Huawei inapanga kuanzisha maduka 5 kabla mwisho wa mwaka huu. Wakati kampuni ya Huawei ilipoanza kuingia kwenye soko la simu za mkononi za kisasa, ilichagua watoa huduma za mitandao ya simu kuwa wenzi wa ushirikiano, lakini haikupata mafanikio. Baada ya kufanya uchunguzi na kuiga uzoefu wa washindani, kampuni ya Huawei hivi sasa inachukua njia vingi za uuzaji zinazoshirikisha waendeshaji wa mitandao ya simu, na duka maalumu na wafanyabiashara wa soko. Anasema,

    "Hapo awali tuliuza simu za mkonoi kwa watoa huduma za mitando ya simu kama Econet, Netone na Telone, lakini baadaye tuligundua lazima tuingie soko la kufungua, simu za Samsung pia zinauzwa kwa kupitia mfumo huo. Hivyo hivi sasa tunafanya ushirikiano na wafanyabishara wa soko la kufungua. "

    Hivi sasa Huawei inafanya ushirikiano na maduka ya nguo ya Edgar, Trueworth na OK supermarket, na imeanzisha sehemu zinazouza simu za mkononi kwenye maduka hayo. Hadi sasa idadi ya maduka ya ushirikiano na Huawei imezidi mia moja.

    Maneja Lai Cuihai amesema kampuni ya Huawei inatilia maanani sana umuhimu wa wafanyakazi wa huko. Hivi sasa asilimia 60 ya wafanyakazi nchini humo ni wazimbabwe, ambao wamezoea mazingira, sera na masoko ya huko, hiyo inaisaidia kampuni ya Huawei kuzoea soko la huko mapema. Anasema,

    "Asilimia 60 ya wafanyakazi wa kampuni yetu nchini Zimbabwe ni watu wa huko, na wenzi wetu wa ushirikiano wote ni kampuni za huko. Tulipojenga kituo cha msingi cha mtandao wa simu, kampuni zilizoshughulikia ujenzi wa miundombinu, uundaji wa mashine na zana, na ununuzi wa vifaa, zote ni kampni za Zimbabwe. Wakati huo huo tulianzisha mradi uitwayo watu wenye ujuzi wa siku za baadaye, tumetoa mafunzo kwa raia wa Zimbabwe. Mradi huo utaendelea kuimarishwa baadaye, tunaweka akiba ya watu wenye ujunzi kwa maendeleo ya kampuni yetu, hii pia ni kuandaa watu wenye ujuzi kwa Zimbabwe."

    Kampuni ya Huawei pia inakabiliwa na changamoto nyingi nchini Zimbabwe, kwa mfano kudidimia kwa uchumi wa Zimbabwe, upungufu wa uwezo wa wanunuzi, kuongezeka kwa ushuru wa kuagiza simu za mkononi, na sera zisizo wazi za huko. Maneja Lai Cuihai anasema,

    "Ikiwa kampuni moja ya kimataifa inayofanya biashara duniani, kama lengo letu ni kufanya biashara katika kila nchi na kumhudumia kila mtu, ni lazima kwetu kukabiliana na changamoto pamoja na watu wa huko. Tuna imani kuwa tukifanya juhudi tutapata utatuzi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako